Na Mwandishi wetu, Babati
MGOMBEA ubunge wa Jimbo la Babati Mjini Mkoani Manyara kwa tiketi ya CHAUMMA mhandisi Joseph Shayo amewaomba wakazi wa eneo hilo kumpa kura za ndiyo ili awatumikie kwa nguvu zake zote.
Mhandisi Shayo ameyasema hayo mara baada ya kurejesha fomu za kuomba kuteuliwa kugombea ubunge wa Jimbo la Babati Mjini.
“Matarajio yangu nikushinda kwa kishindo mimi pamoja na mgombea wangu wa uraisi kupitia chama cha ukombozi wa umma (CHAUMMA) Salimu Mwalimu katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 na kwenda kukabidhiwa dola,” amesema Eng Shayo.
“Ninatamani kuona vijana wakiinuka kiuchumi kwa kuajiriwa na kujiajiri, sababu siyo vizuri kuona mzazi anavyotaabika kupata kipato leo, ili amsaidie mwanaye kupata elimu bora na mwisho wa siku mwanae anakuja kuishia kuwa mlevi na mzururaji wa mitaani,” amesema Eng Shayo.
Mhandisi huyo amesema kimsingi Serikali inapaswa kuwasaidia vijana hususani mitaji ili waweze kufanya biashara zitakazo wasaidia kujikimu kimaisha.
Ameeleza kwamba ili hilo lifanikiwe anapaswa kuwepo mtu sahihi mwenye uchungu na maisha, atakaye kwenda kulisimamia kule Bungeni.
Pamoja na mambo mengine tumeona Serikali ya CCM Ikiwawezesha vijana pamoja na baadhi ya vijana kujiwezesha wenyewe kwenye miradi ya bodaboda, lakini niseme kweli mimi ni dereva boda na mhanga wa polisi wanavyo wapeleka mputamputa, bodaboda huko mtaani,” amesema.
Amedai kwamba anatamani ashinde kwenye huu uchaguzi ili aweze kwenda kuwasemea kwa niaba ya bodaboda wote Tanzania kwani hilo siyo la Babati pekee bali nchi nzima.
Amesema pamoja na bunge kuwapunguzia adhabu za faini, kutoka shilingi 30,000 kwa kosa moja mpaka shilingi 10,000 kwa kosa moja bado askari wa polisi kwa maana ya trafiki wamekuwa wakiwapiga faini nyingi kwa wakati mmoja mpaka makosa manne bila onyo ila vyombo vikubwa vya moto hupigwa faini moja na kuachiliwa.
“Je hawa vijana Serikali inawasaidia au imewafanya mtaji, hivyo baada tu ya kuapishwa huu utakuwa mtaji wangu, tumeendelea kushuhudia ndugu zetu wengi wakiuawa, kupigwa, kutekwa, kupotea na watu wasiojulikana, jukumu langu la pili baada ya kuaoishwa, nikwenda kuihoji Wizara ya Mambo ya Ndani kwa polisi ni wapi walipo ndugu zetu waliopotea, na kushinikiza ripoti za waliouawa ziwekwe wazi tujuwe ni nani hawa wauaji na watekaji?” amehoji.
“Mwisho siyo kwa kumalizia kila mwaka bajeti ya vijana wanawake na watu wenye ulemavu inatengwa, hoja yangu ya msingi ni ipi hapa?
kwanini haya makundi yanapo wezeshwa wasiachiwe kama mtaji na badala yake huishia kurejesha ilihali nchi yetu ina hazina nyingi kweli na makundi haya hawana pengine wanapo nufaika,” amesema.
“Hawana kiinuwa mgongo, ,hawana posho, hawana mshahara, hawana bima nilini nao watanufaika na neema za nchi hii? nitakapofika Bungeni nitakwenda kuyasimamia na mengine mengi kwani ukizungumzia changamoto za watanzania ni zaidi ya kitabu,” amesema.
“Wana Babati ninawaalika mnichague kwa kishindo nawaalika na wa Tanzania waichague Chaumma ili tuweze kwenda kushikamana katika kusimamia haya na mengine mengi, asanteni sana mhandisi Joseph Shayo mgombea ubunge Jimbo la Babati mjini,” amesema Shayo.