NA DENIS MLOWE, IRINGA
MGOMBEA ubunge jimbo la Kilolo na mwanamke Pekee mkoa wa Iringa kugombea ubunge, Rita Kabati amefunika katika zoezi la uchukuaji fomu kwa kupata wadhamini wengi kutoka Chama Cha Mapinduzi .
Kabati anbaye alisindikizwa na makada mbalimbali akiwemo pacha wake Venance Mwamoto aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo hilo alichukua fomu huku umati wa wananchi wa jimbo wakishuhudia zoezi hilo.
Rita Kabati ambaye kabla ya kuchukua fomu kugombea jimbo amekuwa mbunge viti maalum mkoa wa iringa kwa miaka 15 hivyo kumwezesha kuwa mbunge mwenye uzoefu bungeni na CCM kumwamini kuwa mwakilishi pekee wa jimbo la Kilolo mkoani Iringa ambaye ni mwanamke wa shoka.
Akizungumza baada ya kuchukua fomu Dkt. Kabati aliwashukuru viongozi wa CCM kwa imani waliyoonesha kwake na kutoa wito wa mshikamano miongoni mwa wanachama wa chama hicho akisema huu ni wakati wa kuvunja makundi na kuungana kwa pamoja kuhakikisha ushindi wa CCM kuanzia ngazi ya udiwani, ubunge hadi urais.
“Naomba makundi yaliyokuwepo yavunjwe, tushikamane kwa pamoja kama wana-CCM ushindi wa chama chetu unategemea mshikamano wetu hivyo tupambane tupate kura za kishindo kwa wabunge wote na kura za Rais.”alisema
Tuwaunge mkono madiwani wetu, mgombea urais na chama kwa ujumla kwa kura za kishindo,” alisema Dkt. Kabati.
Kwa muda wa miaka 15 akiwa mbunge wa Viti Maalum Dkt. Kabati amejipatia sifa ya kuwa mtetezi wa masuala ya wanawake, wenye ulemavu ,watoto na maendeleo ya jamii kwa ujumla kwa kutoa misaada mbalimbali katika mkoa wa Iringa.

