Afisa Mtendaji Mkuu wa Mkapa Foundation Ellen Mkondya Senkoro akimuelekeza jambo Mwakilishi wa WHO nchini Tanzania Dr. Tigest Ketsela katikati wakati alipotembelea banda la taasisi hiyo katika maadhimisho ya Siku ya Madaktari Tanzania yaliyofanyika jana kwenye ukumbi wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mkapa Foundation Ellen Mkondya Senkoro akiwa na Mwakilishi wa WHO nchini Tanzania Dr. Tigest Ketsela kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es salaam walipotembelea banda la Mkapa Foundation katika maadhimisho hayo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mkapa Foundation Ellen Mkondya Senkoro kulia na Mwakilishi wa WHO nchini Tanzania Dr. Tigest Ketsela wakifurahia jambo, Kushoto ni Rebeca Stanley
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mkapa Foundation Ellen Mkondya Senkoro wa pili kutoka kushoto akiwa na Rahel Sheiza Mkurugenzi wa Miradi pamoja na baadhi ma maofisa wa taasisi hiyo kutoka kulia ni Christina Godfrey Afisa Sera na Uraghbishi Mkapa Foundation , Rebeca Stanley Afisa Uhusiano na Mawasiliano Mkapa Foundation na kushoto
Rahel Sheiza Mkurugenzi wa Miradi Mkapa Foundation katikati akiwa na Rebeca Stanley Afisa Uhusiano na Mawasiliano Mkapa Foundation kushoto na Christina Godfrey Afisa Sera na Uraghbishi Mkapa Foundation.
……………………………………………..
RAIS Dkt. John Magufuli ameameipongeza taasisi ya Mkapa Foundation kwa kujenga nyumba za madaktari 482 nchini kote ikiwa na jitihada za taasisi hiyo kutatua changamoto zinazoikabili sekta ya afya nchi Tanzania
Akizungumza Alhamisi (Februari 20, 2020) Jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya siku ya Madaktari Tanzania yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam , Rais Magufuli alisema naipongeza taasisi ya Mkapa Foundation kwa kuwa mstari wa mbele katika kusaidiana na serikali kutatua matatizo mbalimbali yanayoikabili sekta ya afya nchini.
“Serikali ya Awamu ya Tano itaendelea kutoa kipaumbele katika kuimarisha mifumo ya utoaji wa huduma bora za afya nchini ili kuimarisha ustawi wa maisha ya wananchi na Watanzania kwa ujumla ikiwa ni pamoja na kushirikiana vizuri na taasisi zinazofanya kazi ya kusaidiana na serikali kutatua matatizo mbalimbali katika sekta ya afya”.Amesema Rais DK. John Pombe Magufuli.
Taasisi ya Mkapa Foundation katika mkakati wake wa kupunguza changamoto za sekta ya afya pamoja na kujenga nyumba hizo katika vituo 268 nchini kote pia imejenga vyumba 11 vya upasuaji katika vituo 12 vya kutolea huduma ambapo ujenzi huo umeambatana na kuweka vifaa, kuajiri watumishi na kutoa mafunzo stadi kwa watumishi.
Mkapa Foundation imetoa ajira 2033 za wataalamu wa afya Kada mbalimbali 11 waliopangiwa kazi katika mamlaka za Serikali za Mitaa 51 katika mikoa 22 na vyuo vya Afya 46 ambapo mpaka sasa watumishi 1397 wameshahusishwa katika utumishi wa umma.