Timu ya Taifa ya Tanzania, maarufu kama Taifa Stars, imefanikiwa kutoka sare ya bila kufungana (0-0) dhidi ya timu ya Taifa ya Jamhuri ya Afrika ya Kati katika mchezo wa mwisho wa Kundi B wa michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN 2024)
Mchezo huo umechezwa leo, Agosti 16, 2025, kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam.
Kwa sare hiyo, Taifa Stars imejikusanyia pointi moja muhimu iliyoiwezesha kumaliza kileleni mwa Kundi B ikiwa na jumla ya pointi 10. Tanzania imeshinda michezo mitatu na kutoa sare mmoja kati ya minne ya hatua ya makundi, na hivyo kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano hiyo kwa kishindo.
Mashabiki wa soka nchini wameipongeza timu hiyo kwa kuonyesha kiwango bora na kuendelea kuipeperusha vyema bendera ya taifa.