Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi,akizungumza kabla ya mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo kuzindua shule shikizi ya Msingi Chiwondo iliyopo kata ya Nala jijini Dodoma.
Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, kazi, vijana na Ajira,ambaye pia ni Mbunge wa Dodoma mjini Mhe. Anthony Mavunde,akizungumza na wananchi katika uzinduzi wa shule shikizi ya Msingi Chiwondo iliyopo kata ya Nala jijini Dodoma ambapo asilimia kubwa aliyefanikisha ujenzi huo ni yeye Mhe.Mbunge.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo,akiwatunza wanakwaya pesa ambao walikuwa wakitoa burudani katika uzinduzi wa shule shikizi ya Msingi Chiwondo iliyopo kata ya Nala jijini Dodoma ambapo asilimia kubwa aliyefanikisha ujenzi huo ni Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Mhe. Anthony Mavunde.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo,akizungumza kwenye uzinduzi wa shule shikizi ya Msingi Chiwondo iliyopo kata ya Nala jijini Dodoma ambapo asilimia kubwa aliyefanikisha ujenzi huo ni mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Mhe. Anthony Mavunde.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo,akiwa katika picha na Mkurugenzi Mtendaji wa Glaring Future Foundation(GFF), Bi. Aisha Msantu ambaye ametoa msaada wa madawati 60.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo,akizindua rasmi shule shikizi ya msingi Chiwondo iliyopo kata ya Nala jijini Dodoma ambapo asilimia kubwa aliyefanikisha ujenzi huo ni mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Mhe. Anthony Mavunde.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe Selemani Jafo (katikati) akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge (kushoto) na Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Anthony Mavunde kwenye moja ya madarasa ya shule shikizi iliyozinduliwa leo.
PICHA NA ALEX SONNA-FULLSHANGWEBLOG
………………………………………………………………………………………………………………
Na. Majid Abdulkarim
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Mhe.Selemani Jafo amemtaka Mkurugenzi wa jiji la Dodoma Godwin Kunambi kuhakikisha anajenga nyumba za walimu kwa wakati katika shule ya Msingi Chiwondo .
Agizo hilo amelitoa leo katika Uzinduzi wa shule shikizi ya Msingi Chiwondo iliyopo kata ya Nala jijini Dodoma iliyojengwa kwa msaada wa Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Mhe Anthony Mavunde kwa kushirikiana na Halmashauri ya Jiji hilo ambapo tayari vyumba vinne vya madarasa vimeshakamilika huku vingine vitatu vikiwa kwenye ujenzi.
Mhe. Jafo amesema kuwa ujenzi wa nyumba za walimu zikamilishwe kwa haraka na zijengwe kwa ubunifu mkubwa ili kuweza kupokea walimu wakutosha watakao patikana kuhudumu katika shule hiyo.
“Nimesikia kuna walimu wawili katika shule hii, Walimu hawa wanatembea mwendo mrefu kuja kufundisha hapa hivyo mnaweza kuona jinsi gani wametanguliza uzalendo mbele katika kulitumikia taifa hili” amesema Mhe. Jafo
Waziri Jafo amemwelekeza Mkurugenzi wa Elimu TAMISEMI, Bwana Julius Nestory kabla ya mwezi wa sita mwaka huu kuwa amepeleka fedha za ujenzi wa vyumba vya madarasa vili ili ifikapo mwakani 2021 wanafunzi wote kuwa wamehacha kutembea mwendo mrefu kufata elimu katika shule za mbali.
Mhe. Jafo amesema lengo la kuongeza vyumba vya madarasa ni kutaka ifikapo mwakani 2021 wanafunzi wote wahamie katika shule hiyo na kuhacha kutembea umbali wa mwendo mrefu jambo lilikuwa likisababisha utoro shuleni.
Pia Mhe.Jafo amesema kuwa shule hiyo itapewa kipaumbele cha kupatiwa walimu pale wakati ajira zitakapo tangazwa ili kuongeza nguvu kazi kwa walimu wawili ambao tayali wapo katika shule ya Chiwondo.
“Nawapongeza wananchi waliyojitolea ekali kumi ili kufanyikisha ujenzi wa shule hii, ila nitoe wito kuwa mwendelee kujitolea kwani tunahitaji kujenga sekondari na zahanati au kituo cha afya katika kata hii hivyo tunaomba ushirikiano wenu ili kufanyikisha adhima hii kwani jukumu letu ni kuwahudumia watanzania na kila kata kuwa na huduma za msingi za kijamii” ameeleza Mhe. Jafo
Mhe. Jafo amesema kuwa atamuagiza Mkurugenzi wa TARURA kwenda kufanya uchunguzi na tathimini ya Barabara ya kufika shuleni hapo ili baadaye iweze kufanyiwa ukarabati na Watoto waweze kufika shuleni bila kikwazo chochote.
Kwa upande wake Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde ambaye pia ni Mbunge wa Dodoma mjini amesema kufikia 2021 shule zote za msingi sitakuwa zimepatiwa umeme ili kuweza kutumia kompyuta katika kuboresha sekta ya elimu katika kuunga juhudi za Serikali ya Awamu ya tano katika sekta ya elimu.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk.Binilith Mahenge ametoa wito kwa wazazi na walezi wa wanafunzi kutoa ushirikiano kwa kuhakikisha wanafunzi wanafika shuleni na kuendelea kuchangia katika kuboresha miundombinu ya shule hiyo.
Pia Mkurugenzi wa jiji la Dodoma Godwini Kunambi amesema kuwa ametoa pikipiki mbili kwa walimu wa wili wanao hudumu katika shule hiyo huku akiweka wazi kuwa ofisi yake inaweka utaratibu mzuri wa kuweza kuwajengea jingo la utawala na nyumba za walimu ili kuepuka adha ya kutembea mwendo mrefu.
Lakini pia mmoja wa wadau wa maendeleo Mkurugenzi Mtendaji wa Glaring Future Foundation (GFF), Bi. Aisha Msantu katika uzinduzi huo amechangia madawati 60 na kutoa wito kwa wananchi kuchangia miundombinu ya shule ili Watoto waweze kupata elimu bora katika mazingira sahihi.
Shule ya Chiwondo ina walimu wawili na kila mwalimu anafundisha madarasa mawili, shule hiyo kwa sasa ina vyumba vinne vya madarasa huku vingine vitatu vikiwa mbioni kukamilika na shule inawanafunzi 60 wa darasa la kwanza hadi la nne.