Home Mchanganyiko BASHUNGWA: TUUNGE MKONO BIDHAA ZA NDANI ‘MADE IN TANZANIA’

BASHUNGWA: TUUNGE MKONO BIDHAA ZA NDANI ‘MADE IN TANZANIA’

0

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe.Innocent Bashungwa akizungumza
na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhuhu bidhaa za kiwanda cha vifaa vya
umeme cha Africab Jijini Dar es Salaam kinachozalisha vifaa mbalimbali ikiwemo
transfoma, katika mwendelezo wa Ziara ya kutembelea viwanda Jijini Dar es
Salaam.

Baadhi ya Vifaa vya Umeme vinavyozalishwa na kiwanda cha Africab
kilichopo Jijini Dar es salaam, kiwanda hicho kinatengeneza vifaa mbalimbali
zikiwemo transfoma na nyaya za umeme.

Moja ya Transfoma inayotengenezwa na Kiwanda cha Africab kilichopo
Jijini Dar es salaam, ambapo Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe.Innocent
Bashungwa alitembelea na kutoa rai kwa watanzania kutumia bidhaa zitokanazo na
viwanda vya ndani.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe.Innocent Bashungwa, Katibu Mkuu wa
Wizara hiyo, Prof. Riziki Shemdoe na wamiliki wa kiwanda kuzalisha vifaa vya
Umeme cha Tropical kilichopo Dar es Salaam, Bw.Charles Mlawa na Aloyce Ngowi
baada ya kutembelea kiwandani hapo leo Februari 19, 2020 katika Mwendelezo wa
ziara ya kutembelea viwanda Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe.Innocent Bashungwa, Katibu Mkuu wa
Wizara hiyo, Prof. Riziki Shemdoe wakisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa
Kiwanda cha Tropical kilichopo Dar es Salaam, Bw. Aloyce Ngowi walipotembelea
kiwandani hapo leo Februari 19, 2020 katika Mwendelezo wa ziara ya kutembelea
viwanda Jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya mashine za kutengeneza vifaa vya umeme zilizopo
katika kiwanda cha Tropical kilichopo Jijini Dar es Salaam kama zinavyoonekana
kwenye picha kiwanda hicho kinatengeneza vifaa mbalimbali zikiwemo transfoma,
nyaya za umeme na soketi za umeme.

Mashine ya kusokota nyaza umeme iliyopo katika kiwanda cha
Tropical kilichopo Jijini Dar es Salaam kama inavyoonekana kwenye picha, kiwanda
hicho kinatengeneza vifaa mbalimbali zikiwemo transfoma, nyaya za umeme na
soketi za umeme.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe.Innocent Bashungwa, Katibu Mkuu wa
Wizara hiyo, Prof. Riziki Shemdoe wakisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa
Kiwanda cha Tropical kilichopo Dar es Salaam, Bw. Aloyce Ngowi jinsi ya
kutengeneza transfoma walipotembelea kiwandani hapo leo Februari 19, 2020
katika Mwendelezo wa ziara ya kutembelea viwanda Jijini Dar es Salaam.

Wafanyakazi kutoka kiwanda cha kutengeneza vifaa vya
umeme cha Tropical kilichopo Jijini Dar es Salaam, wakitenegeneza Transfoma
baada ya Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe.Innocent Bashungwa kutembelea
kiwanda hicho katika mwendelezo wa ziara ya kutembelea viwanda Jijini Dar es
Salaam.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe.Innocent Bashungwa, akisalimiana na
Mfanyakazi wa kiwanda cha Tropical katika kitengo cha kutengeneza soketi katika
kiwanda hicho kilichopo Jijini Dar es Salaam.

Transfoma na Vifaa vingine vya umeme kutoka kiwanda cha Tropical
ambapo Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe.Innocent Bashungwa alitembelea
katika mwendelezo wa ziara ya kutembelea viwanda Jijini Dar es Salaam kama
vinavyoonekana kwenye picha.
Picha na Idara ya Habari-MAELEZO.

……………………………………………………………………………………………………

Na. Eric Msuya – MAELEZO

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa amewataka
wadau wa Viwanda na Biashara kuendelea kuunga mkono Serikali ya
awamu ya tano kwa kuendelea kutoa ajira katika viwanda vidogo na
vikubwa ili kupunguza adha ya ukosefu wa ajira kwa vijana Nchini.

Ameyasema hayo leo Jumatano katika mwendelezo wa ziara yake ya
kutembelea Viwanda vilivyopo Jijini Dar es salaam na kutoa rai kwa
kwa watanzania kutumia bidhaa zinazotokana na viwanda vya ndani ili
kuongeza ajira kwa vijana

“Hongereni kwa kumuunga mkono Rais wetu Magufuli kwa kuwapa ajira
watanzania 150, ambao ni wahitimu wa vyuo mbalimbali hapa nchini,
lakini hata wale walikuwa nyumbani wamekaa bila kazi” alisema Mhe.
Bashungwa
Katika Ziara hiyo Mhe. Bashungwa amewapongeza Bwana Charles
Mlawa na Aloyce Ngowi ambao ni wamiliki wazawa wa kiwanda cha
Tropical kilichopo Jijini Dar es Salaam kinachozalisha Vifaa vya Umeme
(Soketi na Transfoma) hapa Nchini kwa lengo la kuunga mkono Serikali
kufikia Uchumi wa kati wenye viwanda.
“Nyie ni wazalendo, ni mfano tosha kwa wawekezaji wazawa kwa
kufahamu umuhimu wa Serikali kufikia uchumi wa kati, transfoma na
nyanya za kupitishia umeme zote zenye ubora sasa zinatengenezwa
Tanzania tena mwenge, Dar es Salaam, na sio tena kuagiza kutoka nje
ya Nchi” alisema Mhe. Bashungwa
aidha Mhe. Bashungwa alitoa rai kwa wananchi na wadau wa sekta ya
Viwanda na Biashara kuendelea kuunga mkono kwa kununua bidhaa za
ndani zinazo tengenezwa na wawekezaji wazawa na wazalendo.
“Niwaombe watanzania kuendelea kuipa kipaumbele neno ‘MADE IN
TANZANIA’ utajisikiaje umeenda Nchi za watu ukakuta chombo
unachotumia kimewekwa nembo ya Tanzania, hakika ni fahari sana”
alisema Mhe. Bashungwa
Naye Mkurugunzi Mkuu wa kiwanda cha Tropical, Ndugu Charles Mlawa
ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuendelea kuwaunga mkono na
kuwajali katika kuhakikisha sera na lengo la kufikia uchumi wa kati

Nchini ifikapo 2025, kwani mpaka sasa kiwanda hicho kinapata umeme
wa uhakika kutoka Tanesco.
“Nampongeza sana Rais Magufuli kwa kuendelea kutuunga mkono sisi
wawekezaji wa ndani, kwetu sisi ni fahari na tutaendelea kuiunga
mkono Serikali yetu” alisema Bwan. Mlawa
Waziri Bashungwa katika ziara yake, pia alitembelea kiwanda cha
AFRICAB kilichopo Kurasini Jijini Dar es Salaam kinacho jihusisha na
utenegezaji wa vifaa vya umeme vya majumbani, kinachomilikiwa na
Wageni kutoka India.