RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Dk. Ali Mohamed. Shein akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, wakati wa kuwasilisha Utekelezaji wa Mpango Kazi kwa mwezi wa Julai hadi Disemba 2019 /2020, uliofanyika ukumbi wa Ikulu leo 19-2-2020, Jijini Zanzibar.
WAKURUGENZI wa Idara na Mashirika ya Wizara ya Habari wakifuatilia mkutano huo wa uwasilishaji wa Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Wizara yao kwa mwezi wa Julai hadi Disemba 2019 /2020, uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
MAOFISA wa Idara na Mashirika ya Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, wakifuatilia taarifa ya Utekelezaji wa Mpango Kazi kwa mwezi wa Julai hadi Disemba 2019 /2020, wakati ikiwasilishwa taarifa hiyo na Katibu Mkuu.Bi. Khadija Bakari Juma(hayupo pichani)
WAZIRI wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe. Mahmoud Thabit Kombo akiwasilisha muktasari wa Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango Kazi kwa mwezi wa Julai hadi Disemba 2019 /2020, (kulia) Naibu Waziri wa Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar.Mhe. Choum Kombo Khamis.
WAZIRI wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe. Mahmoud Thabit Kombo akiwasilisha muktasari wa Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango Kazi kwa mwezi wa Julai hadi Disemba 2019 /2020, (kushoto )Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee na (kulia) Naibu Waziri wa Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar.Mhe. Choum Kombo Khamis
MKURUGENZI Idara ya Habari Maelezo Zanzibar Dkt. Juma Mohammed Salum akijibu swali wakati wa mkutano wa Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya Kale, kwa mwezi wa Julai hadi Disemba 2019 /2020, uliofanyika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar, ukiongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein.(hayupo pichani)
KATIBU Mkuu Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar.Bi. Khadija Bakari Juma, akiwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Mpango Kazi kwa Wizara yake kwa mwezi wa Julai hadi Disemba 2019 /2020, uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar, kushoto Naibu Katibu Mkuu Dkt. Saleh Yussuf Mnemo.
AFISA Mipango wa Shirika la Magazeti la Zanzibar Leo Bi. Wanu Ali Makame akijibu swali wakati wa mkutano wa Utekelezaji wa Mpango Kazi kwa mwezi wa Julai hadi Disemba 2019 /2020.(Picha na Ikulu)