Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mauritania katika mchezo wa michuano ya CHAN 2024 uliochezwa leo, Agosti 6, 2025, kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam.
Bao pekee la Taifa Stars lilifungwa na Shomari Kapombe katika dakika ya 89 ya mchezo, na kuiwezesha Tanzania kujikusanyia pointi tatu muhimu, ushindi ambao unaifanya Taifa Stars kufikisha pointi sita na kuongoza kundi B.
Mchezo unaofuata kwa Taifa Stars utakuwa dhidi ya Madagascar Agosti 9, 2025, ambapo Madagascar kwa sasa inashika nafasi ya tatu katika kundi hilo ikiwa na pointi moja.