****************************
NA MWAMVUA MWINYI,BAGAMOYO
WATU zaidi ya 25,319 wamejitokeza kujiandikisha na wengine kuweka kumbukumbu zao sahihi ,katika zoezi la kuboresha daftari la kudumu la wapiga kura,wilayani Bagamoyo ,mkoani Pwani.
Aidha ,katika zoezi hilo kulijitokeza changamoto ndogo ndogo upande wa mashine za BVR ,lakini ushirikiano ulikuwepo katika kutatua changamoto zinapojitokeza kupitia wataalamu mbalimbali wa TEHAMA na kutoka Tume ya Taifa ya uchaguzi .
Akitoa taarifa hiyo, wakati wa baraza la madiwani ,Halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo ,mwenyekiti wa halmashauri hiyo Ally Ally Issa alisema, vituo vilivyopo wilayani hapo ni 126 ambapo hakuna changamoto kubwa iliyoripotiwa kukwamisha zoezi tangu lianze .
Aliwahamasisha vijana waliofikia umri wa miaka 18 mwaka huu ,wasipuuzie zoezi hili ,wajitokeze kwa wingi ili kupata fursa ya kumpigia kura kwakuwa ni haki ya msingi.
“Ukifikia siku ya nne ya zoezi wamejitokeza watu 25,319, nawasihi walengwa waendelee kujitokeza kwa wingi,waliohama eneo moja hadi jingine, waliopoteza vitambulisho vyao, waliofikisha miaka 18,”
” ,Lengo kubwa halina kificho ,tujitokeze ili kupeleka kura za kishindo kwa Rais John Magufuli ,hakuna haja ya kupindisha maneno maana hakuna asiyeona kama Tanzania imepiga hatua kubwa kiuchumi na kimaendeleo ndani ya miaka mitano ya uongozi wake, Kura zisiwe za kuzitafuta Rais Magufuli apigiwe kura za kutosha ili aendeleze jahazi”aliongeza Ally .
Nae katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bagamoyo, Salum Mtelela alitoa wito hususan kwa vijana kuacha kufanya ajizi katika fursa hiyo adhimu ili kuweza kumpigia kura Rais, mbunge na diwani katika maeneo yao husika.
Alisema, pasipo kuwa na kichinjio ni kazi bure hivyo walengwa wajitokeze ili kutimiza haki yao ya msingi ya kupiga kura.
“Tunataka kura za sunami kwa mwenyekiti wetu Taifa wa CCM ,wabunge na madiwani, maana wembe ni ule ule kama uchaguzi wa serikali za mitaa,vijiji na vitongoji,CCM iibuke kidedea ,hivyo kama kichinjio ukiwa huna utapunguza kura “alihamasisha Mtelela.
Wakazi wa Bagamoyo, waliojitokeza kuweka kumbukumbu zao kwenye zoezi hilo, Riziki Kadiri, Abdul Ally na Martha Thomas walisema ,zoezi hilo halina kero ya foleni ,wala vipingamizi ndio maana limefanikiwa tofauti na vitambulisho vya Taifa-NIDA.
Riziki alisema ,awali alikuwa akiishi Matipwili na sasa kahamia Bagamoyo ,kutokana na kuhama kata amekwenda kujiandikisha katika kata anayoishi sasa ili aweze kumpigia kura Rais,diwani na mbunge.
Nae Abdul alieleza ,baadhi ya watu wanapuuzi kutokana na kujiwekea kuwa watapiga kura kwa Rais pekee,kwani ndio wanaemtaka wengi arudi ili kuinua maendeleo zaidi ,lakini wananchi wanapaswa kuelewa kuna umuhimu pia wa kupata majifya matatu hasa ya chama kimoja ili kupata maendeleo hayo kirahisi