Na Meleka Kulwa – Dodoma
Wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum wa Jumuiya ya wanawake wa Chama Cha Mapinduzi CCM (UWT) Taifa wamemchagua Mwenyekiti wa Kamati ya Ukatili UWT Mkoa wa Mwanza, Bi. Halima Idd Nassor ,kuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia kundi la Wanawake kutoka vyama vyama vya Wafanyakazi Tanzania Bara.
Katika Uchaguzi huo uliofanyika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma, Bi. Halima Idd Nassor amepata ushindi wa kishindo kwa kujizolea kura 566 , na hivyo kuibuka kinara miongoni mwa wagombea waliokuwa wakigombea nafasi hiyo muhimu ya uwakilishi wa kundi la Wanawake kutoka vyama vya Wafanyakazi ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, huku mpinzani wake wa Karibu Mariam Anzuruni Mangula akipata kura 290, kwa upande wa wawakilishi kutoka Zanzibar Visiwani Tunu Juma Kondo amepata Kura 566.
Zoezi la upigaji kura lilianza rasmi mnamo Agosti 2, 2025 na kufikia tamati alfajiri ya Agosti 3, likihitimisha hatua muhimu ya kuwapata wawakilishi wa kundi la Wanawake kutoka vyama vya Wafanyakazi kwa mwaka huu.
kupitia ushindi huo unatoa ishara ya kuaminiwa kwake na Jumuiya ya Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) , pamoja na mchango wake katika harakati za kuwajali na kuwapambania watu ndani ya chama na jamii kwa ujumla.