Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Jaji wa Rufani, Mhe. Jacobs Mwambegele akizungumza katika Mkutano wa Tume na Wazalishaji Maudhui Mtandaoni, uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam, Agosti 3, 2025. Picha na INEC.
Mkurugenzi wa Uchaguzi, Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Ramadhani Kailima akiwasilisha mada ya Maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025, katika Mkutano wa Tume na Wazalishaji Maudhui Mtandaoni, uliofanyika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam, Agosti 3, 2025.
Baadhi ya Wazalishaji Maudhui Mtandaoni walioshiriki Mkutano wa Tume na waandishi hao, uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam, Agosti 3, 2025. Picha na INEC.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Jaji wa Rufani, Jacobs Mwambegele (Katikati waliokaa), Makamu Mwenyekiti wa Tume, Jaji wa Rufani (Mst), Mhe. Mbarouk Salim Mbarouk (watatu kushoto), Mkurugenzi wa Uchaguzi ambaye pia ni Katibu wa Tume, Ramadhani Kailima (watatu kulia), Mjumbe wa Tume, Mhe. Dkt. Zakhia Mohamed Abubakar (kushoto), Mjumbe wa Tume, Mhe. Balozi Omar Ramadhan Mapuri (wapili kushoto), Mjumbe wa Tume, Jaji wa Mahakama Kuu, Mhe. Asina A. Omari (wapili kulia) na Mjumbe wa Tume, Mhe. Magdalena Kamugisha Rwebangira (kulia), wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mkutano wa Tume na Wazalishaji Maudhui Mtandaoni, kufunguliwa katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam, Agosti 3, 2025.
…….
Wazalishaji wa maudhui mtandaoni wametakiwa kuchapisha taarifa sahihi za uchaguzi ambazo hazina chembe ya upotoshaji ili kuepuka kuvuruga na kulinda amani na utulivu wa nchi.
Akizungumza leo 3, 2025, jijini Dar es Salaam, wakati akifungua Mkutano wa Kitaifa kati ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi na wazalishaji wa maudhui mtandaoni kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Jaji wa Mahakama ya Rufani Jacobs Mwambegele, amesema kuwa Tume ina matumaini makubwa na vyombo vya habari katika kufanikisha uchaguzi wa mwaka huu kwa kupitia ushiriki wao wa karibu.
Jaji Mwambegele amesema kuwa ana Imani kubwa na vyombo vya habari kutokana na ushirikiano walionesha tangu awali kwenye zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, huku akisisitiza kuwa waendelea kuwa wepesi wa kuwasilisha hoja na ushauri kila tunapokutana katika vikao mbalimbali.
“Nawakumbusha umuhimu wa kuepuka matumizi mabaya ya akili mnemba, ambayo inatumiwa na baadhi ya watu wenye nia ovu kusambaza habari za upotoshaji, hususan kupitia mitandao ya kijamii,” amesema Jaji Mwambegele.
Nae Mkurugenzi wa Uchaguzi, Ramadhan Kailima, akiwasilisha mada kuhusu maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 na nafasi ya vyombo vya habari, amesewasihi, kutumia nafasi na fursa mlizonazo kuhakikisha kuna kuwepo na taarifa za mara kwa mara kuelezea yanayoendelea kuhusu uchaguzi mkuu.
“Tume inatarajia vyombo vya habari vitatumia kalamu na nyenzo walizonazo kuhubiri amani kipindi chote cha mchakato wa uchaguzi” amesema Kailima.
Amesema kuwa vyombo vya habari vina nafasi ya kuwa sauti ya kwanza katika kubainisha upotoshwaji wa aina yoyote, iwe kwa bahati mbaya au kwa makusudi, kuhusu Tume na mchakato mzima wa uchaguzi.
Amefafanua kuwa tume imeweka utaratibu wa kushirikisha vyombo vya habari katika hatua zote za uendeshaji wa uchaguzi huu, ili kuweka uwazi na kuhakikisha ushiriki wao wa moja kwa moja.
Kura yako haki yako jitokeze kupiga kura.