Na Meleka Kulwa – Dodoma
Jumuiya ya Wanawake ya Chama Cha Mapinduzi (UWT), Chini ya Mwenyekiti wake Bi. Mary Chatanda Leo Agosti 2, 2025 kinatarajia kufanya uchaguzi wa kuwachagua wagombea wa ubunge wa Jumuiya hio katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete uliopo Jijini Dodoma, makundi yanayotarajiwa kupigiwa kura Leo ni kundi la watu wenye ulemavu linajumuisha wagombea watatu kutoka Tanzania Bara na mmoja kutoka Zanzibar. Kundi la wafanyakazi lina wagombea wawili kutoka Bara na mmoja kutoka Zanzibar; wasomi wa vyuo vikuu watatu kutoka Bara na mmoja kutoka Zanzibar; huku kundi la NGOs likiwa na wawili kutoka Bara na mmoja kutoka Zanzibar.
Zaidi ya wanachama 1,200 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar wanatarajiwa kushiriki katika mchakato huo muhimu wa kura za maoni.