Baadhi ya Watumishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali wameshiriki mbio za marathon zijulikanazo kama NBC Dodoma Marathon 2025″.
Watumishi hao wameshiriki katika mbio za kilomita 10 zilizofanyika tarehe 27 Julai, 2025.
Akizungumza kwa niaba ya Watumishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali mara baada ya kukamiliza mbio hizo, Bw. Nicolaus Sitta, ameushukuru Uongozi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kuwawezesha watumishi kushiriki katika mbio hizo.
“Tunawashukuru Viongozi wetu kwa motisha hii ya kutuwezesha kushiriki katika mbio hizi na tunawapongeza kwa juhudi zao za kuhakikisha watumishi wanashiriki katika michezo.”
NBC Marathon 2025 Dodoma imelenga katika kuimarisha mapambanao dhidi ya saratani ya shingo ya uzazi, kuboresha afya ya mama na mtoto na kufadhili wauguzi 100 kwa ajili ya watoro wenye changamoto ya usonji.