Mkuu wa wilaya ya Sumbawanga Nyakia Ally Chirukile wakati akizungumza na wanakamati ya màafa wa wilaya ya Sumbawanga
Mkurugenzi wa menejiment ya màafa kutoka ofisi ya waziri mkuu Brigedia jenerali Hosea Ndagala wakati akizungumza katika uzinduzi wa nyaraka ya màafa
Mwakilishi kutoka Shirika la maendeleo ya kimataifa (UNDP) nchini Tanzania Godfrey Mulisa wakati akiwasilisha mada juu ya màafa na namna ya kujikinga
Kushoto ni mwakilishi wa katibu tawala mkoa wa Rukwa wakati akipokea nyaraka
Baadhi ya wanakamati ya màafa wilaya ya Sumbawanga.
…………..
Na Neema Mtuka Sumbawanga
Rukwa: Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Nyakia Ally Chirukile ameitaka halmashauri ya wilaya ya sumbawanga kusimamia na kutekeleza mpango na mkakati wa Kupunguza Vihatarishi vya Maafa ulioandaliwa na (UNDP) kwa kushirikiana na idara ya maafa kutoka ofisi ya waziri mkuu ili iwe chachu ya ushirikishaji wa jamii na wadau.
Akizungumza leo Julai 24, 2025 Mkuu wa wilaya ya Sumbawanga amesema ili kuimarisha mfumo wa utoaji wa elimu ya tahadhari ya awali ni lazima kujenga uwezo wa kuzuia ,kupunguza madhara ,na kujiandaa kukabiliana na maafa yanayoweza kujitokeza.
Awali akizungumza mara baada ya kuzindua na kukabidhi nyaraka Chirukile katika halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga amesema yale yaliyobainishwa kwenye nyaraka hizo ni majanga ya kweli.
“Haya ni majanga ambayo tunaishi nayo na yamekuwa yakitokea mara kwa mara na hivyo nahimiza wadau wa afya akiwemo mganga mkuu wa wilaya hiyo kuhakikisha unafatilia suala la usafi wa mazingira.” Amesema
Mkuu huyo wa Wilaya ya Sumbawanga amewasisitiza viongozi wa wilaya hiyo kuhakikisha wanafuatiliana na kuhamasisha usafi wa mazingira pamoja na kuhamasisha watu wakae kwenye maeneo bila kutiririsha maji machafu na kuacha kufanya shughuli za kibinaadamu kwenye vyanzo vya maji.
Nae mwakilishi wa katibu tawala wa mkoa wa Rukwa James Kapenulo ameishukru ofisi ya waziri mkuu kitengo cha maafa pamoja na wafadhiri ambao ni Shirika la maendeleo la kimataifa Nchini (UNDP) kwa kuendelea kuwajali wananchi pale wanapopatwa na madhira.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa idara ya menejimenti ya maafa Brigedia Jenerali Hosea Ndagala kwa kushirikiana na halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga kwa ufadhili wa Shirika la maendeleo la kimataifa Nchini (UNDP) amesema lengo la utekelezaji huo ni pamoja na kuweka mgawanyo wa majukumu kwa wadau wote waliopo katika Wilaya ili kuweka mikakati endelevu.
Mwakilishi kutoka Shirika la maendeleo ya kimataifa (UNDP) nchini Tanzania Godfrey Mulisa ameitaka kamati ya màafa ya wilaya hiyo kufanya kazi kwa kushirikiana ili iwe rahisi kukabiliana na maafa yanayotokea hasa kwenye wilaya hiyo.
Baadhi ya washiriki ambao ni wanakamati ya màafa ya wilaya ya Sumbawanga akiwemo Frank Mwaisumbi amesema wilaya hiyo imekuwa ikikumbwa na majanga mbalimbali ikiwemo madaraja kusombelewa na maji hasa nyakati za mvua za masika na majanga mengine likiwemo la ziwa Rukwa.
“Elimu juu ya màafa niliyoipata nitaifanyia kazi kwa kushirikiana na wanakamati na tutawajengea uwezo wananchi kwa kuwapa elimu ya tahadhari ili na wao wasiwe chanzo cha kusababisha majanga bila wao kujua.”amesema MwaisumSumbawanga.