Mtu mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Alptek in Zeynelabidin Aksoy (52) Raia wa Tanzania mwenye asili ya Uturuki ameuawa baada ya kushambuliwa kwa risasi na watu ambao walikuwa wakitumia usafiri wa pikipiki majira ya saa tano na nusu asubuhi eneo la Kinondoni Makaburini, Dar es Salaam,
Wahusika hao inasemekana hawakuchukua kitu chochote baada ya tukio hilo.
Taarifa inasema Alptek in Zeynelabin alishuka kwenye gari lake na kabla ya kuingia ofisini kwake alishambuliwa kwa risasi na kupoteza maisha huku tukio hilo likiacha mashuhuda wakitapata huku na kule kujiokoa
Uchunguzi wa kina kuhusiana na tukio hilo umeanza na Jeshi limetoa onyo kali kwa wote waliohusika kwa sababu zozote zile watakamatwa na kuingizwa kwenye mkondo wa sheria kwa hatua zaidi.