Mkuu wa kitengo cha mawasiliano shirika la Maendeleo ya Petroli na gesi TPDC Maria Mselemu amesema kufuatia utendaji kazi la shirika hilo umewafanya kuibuka kidedea kwenye maonesho ya 49 ya biashara ya kimataifa maarufu kama sabasaba.
Akizungumza mara baada ya kupewa tuzo hiyo katika maonesho ya 49 ya biashara ya kimataifa amesema wamekuwa wakifanya vizuri kwenye maeneo tofauti na kupelekea kupata tuzo mbalimbali.
“Kwetu hii ni tuzo ya tano kwenye maonesho haya lakini sisi kwetu hii ni kawaida kwani tumekuwa tukipata tuzo kwenye maeneo taofauti ikiwemo tuzo ya mazingira”,amesema Mselemu.
Akizungumzia tuzo hiyo ya mazingira amesema kufuatia matumizi ya nishati safi ya kupikia wameweza kuondoa hewa ukaa kwa tani laki moja.
“Kwa kutumia nishati safi ambayo tunaweka kwenye magari lakini pia kupikia pia kufanyakazi kwa umakini ndio kichocheo cha kutufanya kuwa kinara na hata kupatata tuzo kadhaa”ameongeza.