Naibu Kaibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Chrisian Omolo, akieleza kuhusu umuhimu wa Sera za Kodi kwa maendeleo ya Wananchi, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha kwenye Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (Sabasaba) yenye kaulimbiu ya “Maonesho ya Kibiashara ya Kimataifa Sabasaba, Fahari ya Tanzania”.. Kulia ni Afisa Kumbukumbu kutoka Kitengo cha Pensheni, Wizara ya Fedha, Bi. Stella Mtally.

Naibu Kaibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Chrisian Omolo, akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Habari wa Wizara hiyo, Bw. Joseph Mahumi kuhusu Jarida la Wizara hiyo (Hazina Yetu) ambalo linapatikana kwa nakala ngumu na Laini, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha kwenye Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (Sabasaba).

Naibu Kaibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Chrisian Omolo, akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Mwandamizi wa Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali wa Wizara hiyo, Bi. Farida Manilwa Kuhusu elimu ya Pensheni inayotolewa na Hazina alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha kwenye Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (Sabasaba). Katikati ni Afisa Kumbukumbu kutoka Kitengo cha Pensheni, Wizara ya Fedha, Bi. Stella Mtally.

Naibu Kaibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Chrisian Omolo, akikabidhiwa mfuko wenye nembo ya PSPTB na Afisa Uhusiano kwa Umma na Mawasiliano wa Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Bi. Beatrice Sanga, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha kwenye Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (Sabasaba).

Kaimu Kamishna wa Kitengo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi, Bw. Bashiru Taratibu, akizungumza na wataalamu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha kwenye Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (Sabasaba) yenye kaulimbiu ya “Maonesho ya Kibiashara ya Kimataifa Sabasaba, Fahari ya Tanzania”. Wa pili kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi hiyo, Prof. William Pallangyo.

Kaimu Kamishna wa Kitengo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi, Bw Bashiru Taratibu, akisoma Jarida la Hazina Yetu toleo la Tatu kwa mwaka 2024/2025 baada ya kupata maelezo kutoka kwa Afisa Habari Mkuu kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara hiyo, Bi. Eva Valerian, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha kwenye Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (Sabasaba) yenye kaulimbiu ya “Maonesho ya Kibiashara ya Kimataifa Sabasaba, Fahari ya Tanzania” .

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Chrisian Omolo, akiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa Wizara ya Fedha wanaotoa elimu alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha kwenye Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (Sabasaba) ambayo yameanza tarehe 28 Juni na kutarajiwa kuhitimishwa Julai 13 mwaka huu. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha)