Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi inaendelea kutoa huduma katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba yanayoendelea viwanja vya Mwl Nyerere jijini Dar es Salaam.
Katika maonesho hayo yaliyobeba kaulimbiu ya “Fahari ya Tanzania” Wizara ya Ardhi natoa baadhi ya huduma kama vile Hati Milki za Ardhi kwa aliyekamilisha taratibu za umiliki, Ubadilishaji jina (Deed poll), Ukadiriaji Kodi ya Pango la Ardhi, Uthamini wa Mali zinazihamishika na zile zisizohamishika pamoja na utatuzi wa changamoto za sekta ya ardhi.
Aidha, huduma za sekta ya Ardhi katika manispaa za mkoa wa Dar es salaam Kinondoni, Ubungo, Kigamboni, Ilala, Temeke pamoja na Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya zinapatikana katika banda la Wizara.
Vile vile, elimu kuhusiana na masula ya sekta ya milki, urasimishaji pamoja na namna ya kujiunga na Chuo cha Ardhi Morogoro (ARIMO) katika masomo kwa ngazi ya Astashahada na Stashahada inatolewa na wataalamu sambamba na kutoa fomu za kujiunga na chuo hicho.