Mwamvua Mwinyi, Pwani
Julai 3, 2025
Jumla ya wanachama 93 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamechukua fomu za kugombea ubunge katika majimbo tisa ya Mkoa wa Pwani ambapo kati yao, wanawake ni 22 na wanaume ni 71.
Katibu wa Siasa, Uenezi na Mafunzo wa CCM Mkoa wa Pwani, David Mramba, alitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari Julai 2, 2025, mara baada ya kukamilika kwa zoezi la uchukuaji fomu lililoanza Juni 28, 2025.
Akitolea ufafanuzi juu ya zoezi hilo, Mramba alieleza, katika Jimbo la Kibiti: Jumla ya waliochukua fomu ni 10 , wanaume 9, mwanamke 1.
Jimbo la Mkuranga Waliochukua fomu ni 15 , wanaume 9, wanawake 6.
Mramba alieleza, Jimbo la Kisarawe Waochukua fomu ni 12 – wanaume 10, wanawake 2.
Jimbo la Mafia, waliochukua fomu 6 huku wanaume wakiwa 5 na mwanamke 1.
Aliongeza kusema,Jimbo la Kibaha Mjini waliochukua fomu ni 19 kati yao wanaume 15, wanawake 4, na Jimbo la Kibaha Vijijini wapo 9 ikiwemo wanaume 7 na wanawake 2.
Mramba alieleza kwamba,Jimbo la Bagamoyo Waombaji ni 11 kati hao wanaume 7, wanawake 4 na kwa upande wa Jimbo la Chalinze waliochukua fomu ni 3 wote ni wanaume.
“Huko katika Jimbo la Rufiji wapo 8, ambapo wanaume wapo 6 na wanawake ni 2.
Aidha kati ya waliochukua fomu wamo waliokuwa wabunge kwenye majimbo hao akiwemo alhaj Selemani Jafo-Kisarawe , Ridhiwani Kikwete-Chalinze, Abdallah Ulega-Mkuranga, Mohammed Mchengerwa -Rufiji na Muharami Mkenge -Bagamoyo.
Wengine ni Twaha Mpembenue-Kibiti, Omar Kipanga-Mafia ,Silvestry Koka -Kibaha Mjini na Michael Mwakamo -Kibaha Vijijini.
Vilevile, Mramba alimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan, kwa juhudi kubwa anazoendelea kufanya katika kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika mkoa huo.
Alieleza kuwa, Serikali chini ya Rais Samia imekuwa ikitoa fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo, hali inayoakisi dhamira ya dhati ya kuwaletea wananchi maendeleo ya kweli.
Hata hivyo, Mramba alimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Pwani ambaye pia ni Kamisaa wa Mkoa huo, Alhaj Abubakar Kunenge, kwa usimamizi thabiti wa miradi na ushirikiano alioonyesha kati ya Serikali na Chama, hali iliyochangia mafanikio hayo.