Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, amekutana na Mabalozi wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Ulaya (EU), wanaowakilisha nchi zao nchini Tanzania.
Kikao hicho kilichohusu mashauriano ya kuendelea kuboresha ushirikiano wa muda mrefu na uhusiano wa kidiplomasia baina ya pande mbili hizo, kilifanyika jijini Dar Es Salaam, Jumanne, tarehe 1 Julai 2025.
Mabalozi wa nchi hizo, waliokutana na Balozi Nchimbi, na nchi zao kwenye mabano ni pamoja na Mhe. Balozi Anne-Sophie Avé (Ufaransa), Mhe. Balozi Charlotta Ozaki-Macias (Sweden), Mhe. Balozi Wiebe de Boer (Uholanzi), Mhe. Balozi Sergiusz Wolski (Poland).
Wengine ni Mhe. Balozi Thomas Terstegen (Ujerumani), Mhe. Balozi Jesper Kammersgaard (Denmark), Mhe. Balozi Nicola Brennan (Ireland), Mhe. Balozi Giuseppe Coppola (Italia), Mhe. Balozi Peter Huyghebaert (Ubelgiji), Mhe. Balozi Theresa Zitting (Finland) na Balozi wa EU nchini Tanzania Mhe. Christine Grau.
Mazungumzo hayo ni mwendelezo wa hatua mbalimbali zinazochukuliwa na CCM, kikiwa ni chama kinachotoa uongozi wa nchi, kuhakikisha Serikali na Tanzania, inaimarisha uhusiano wa kidiplomasia na ushirikiano wake na jumuiya ya kimataifa katika masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo na ustawi wa nchi na Watanzania wote kwa ujumla.
Pichani ni Katibu Mkuu wa CCM Balozi Emmanuel John Nchimbi akiwa kwenye picha ya pamoja na mabalozi hao wa EU. Kushoto kwa Dkt. Nchimbi ni Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Rabia Hamid Abdalla.