Na Hellen Mtereko,
Mwanza
Mtia nia nafasi ya Ubunge Jimbo la Ilemela Kafiti William Kafiti amemshukuru Mungu kwa kumjalia afya njema tangu alipochukua fomu Juni 29 hadi leo Julai 02 2025 aliporudisha fomu hiyo.
Kafiti ambae ni mara yake ya pili kutia nia katika Jimbo hilo ameyasema hayo leo Julai 02, 2025 mara baada ya kurudisha fomu kwa katibu wa CCM Wilaya ya Ilemela Hassan Milanga.
“Namshukuru Mungu sana nimefanikiwa kuchukua na kurejesha fomu salama ya kuomba ridhaa ya Ubunge katika Jimbo la Ilemela Mkoani Mwanza nasubili maamuzi ya vikao vya juu na mwenyezi Mungu akijalia nikakiwakilisha chama nitakuwa tayari kutumika katika Jimbo hili la Ilemela”, Amesema Kafiti