Na Mwamvua Mwinyi,Mvomero
Julai 2,2025
Eng. Noah MAHIMBO (SANYANGASI), Achukua fomu ya kuwania ubunge katika Jimbo la Mvomero -Morogoro kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).
Akiongea Baada ya Kuchukua Fomu Eng. Mahimbo ameahidi Kushirikiana na Rais Daktari Samia Suluhu Hassan, Madiwani wa Kata zote za Mvomero, Viongozi wa Chama, wa Serikali na Wananchi wote wa Mvomero katika Kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) 2025-2030 lakini pia katika Kuifanya Mvomero kuwa Mvomero ya Viwanda.
“Kama Chama kikinipa Ridhaa ya Kupeperusha Bendera Katika Uchaguzi Mkuu na hata Kuwa Mbunge, Agenda yangu kuu Moja ni Kuifanya MVOMERO kuwa Wilaya ya Wazalishaji, hapa Tutawekeza katika Kilimo Biashara ndani na Mipaka ya Nchi, sababu Uchuuzi wa Kununulia Mazao yakiwa Ghafi Mashambani yamewafanya Wakulima Kutonufaika na Ongezeko la Thamani ya Bidhaa, MUNGU ametubariki Ardhi hivyo Hatupaswi Kuishia kujilisha wenyewe Tu, ni Lazima tujiweke kwenye Nafasi ya Kulisha Wengine na hapo itatuletea Manufaa ya Kiuchumi”
Lakini jambo la Pili Tutawekeza katika Viwanda vidogo vidogo vingi na Kufanya Mvomero kuwa Miongoni mwa Maeneo yenye Industry per Capita Kubwa hapa Tanzania na hii ni katika kufanya Primary Processing ya Mazao yetu.
“Maono yangu ni kuwa na Mvomero ya Viwanda”