Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Musa Ryoba, ameonesha dhamira ya kulitumikia Taifa kwa kuchukua na kurejesha fomu ya kuomba ridhaa ya chama cha Mapinduzi ili kugombea nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Tarime Mjini, mkoani Mara, katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 2025.
Ryoba amechukua na kurejesha fomu hiyo katika ofisi za CCM Wilaya ya Tarime.
Mussa nimiongoni mwa Vijana ambao tayari wameonesha nia ya kuomba ridhaa baada cha Chama cha Mapinduzi Kutangaza Tarehe ya uchukuaji fomu.
Shughuli ya uchukuaji fomu inaendelea ikitarajiwa kutamatishwa July 2 mwaka huu