Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha
Mgombea wa ubunge Jimbo la Kibaha Mjini Godwin Ndosi amechukua fomu ya kugombea ubunge katika Jimbo la Kibaha Mjini lililopo Mkoani Pwani.
Ndosi ,amechukua fomu hiyo katika ofisi za Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kukabidhiwa fomu hiyo na Katibu wa CCM Kibaha Mjini Isaack Kalleiya.
Akizungumza na Waandishi wa habari mara baada ya kuchukua fomu hiyo Ndosi amesema kuwa anatambua Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini Silvestry Koka amefanyakazi kubwa lakini na yeye anaingia kwa ajili ya kuendeleza pale ambapo Koka ameishia.
“Nimekuja hapa kuchukua fomu na lengo kubwa ni kuleta mabadiliko ya Kibaha Mjini hususani katika kuwaletea Wananchi maendeleo lakini natambua Mbunge Koka kafanya mengi na mimi nitaendeleza pale alipoishia.