Na Mwandishi Wetu
Kampuni ya bia ya Heineken imezindua rasmi chapa yake mpya ya Heineken Silver nchini Tanzania, ikiwa ni mwanzo wa mwelekeo mpya wa burudani mijini wenye hadhi, ubunifu na uzoefu wa kipekee kwa wapenzi wa starehe.
Uzinduzi huo ulifanyika usiku wa Juni 22 kwenye ukumbi wa kisasa uliopo basement ya Mlimani City, jijini Dar es Salaam, na kuhudhuriwa na wageni zaidi ya 400. Tofauti na matukio mengine ya kawaida, tukio hili halikuwa na mgawanyo wa VIP – kila mgeni alihudumiwa kwa viwango vya juu bila ubaguzi, kielelezo cha maono ya Heineken Silver ya burudani jumuishi na ya kisasa.
Kauli mbiu ya #SmoothExperience iliakisiwa vyema katika kila kipengele – kuanzia mazingira yaliyopambwa kwa ustadi, huduma bora, hadi burudani ya nguvu kutoka kwa msanii maarufu Chino Kidd ambaye alichukua jukwaa na kufanikisha usiku wa kusisimua uliowaacha wengi wakitamani zaidi.
Wageni walivaa mavazi ya kuvutia yaliyoakisi kauli ya “Silver Futuristic”, na shindano la vazi bora likazua shamrashamra kubwa. Mshindi wa shindano hilo alizawadiwa kitita cha Shilingi milioni 2, ishara ya kuthamini ubunifu na ushiriki wa wageni.
Kwa wale waliohudhuria, kila kitu kilitolewa bure – vinywaji, vyakula na burudani – likiwa ni jibu kwa kiu ya matukio yenye ubora wa kimataifa, lakini yanayowahusisha watu wote.
Kwa uzinduzi huu, Heineken Silver haikuanza tu kama kinywaji kipya, bali kama harakati mpya ya starehe yenye hadhi jijini. Na bila shaka, huu ni mwanzo wa zama mpya za burudani Tanzania.