Happy Lazaro,Arusha .
Arusha .Waziri wa TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa leo amevunja rasmi mabaraza ya Madiwani hapa nchini huku akitupia sifa madiwani kwa kufanya kazi nzuri na kwa weledi na kuwa kwa kitendo hicho kazi yao imeandikwa kwenye kitabu cha dhahabu.
Aidha Waziri Mchengerwa ameyasema hayo wakati akizungumza kwa simu na baraza la madiwani halmashauri ya jiji la Arusha kupitia simu ya mkuu wa mkoa wa Arusha,Paulo Makonda na kumuunganisha kwa lengo la kuzungumza na madiwani huku akitumia fursa hiyo kuvunja mabaraza yote nchini na kuzungumza na madiwani wote nchi nzima .
“Nakushukuru sana mkuu wa mkoa wa Arusha kwa kuniunganisha na baraza la madiwani la Arusha na kufanya iwe kituo cha kutoa tamko kwa mabaraza yote nchini nimefurahishwa sana na jambo hili.”amesema Mchengerwa.
Waziri Mchengerwa amewashukuru Mameya pamoja na wenyeviti wote wa halmashauri nchini na kusema kuwa mafanikio ya serikali ya awamu ya sita yametekelezwa vyema chini ya mamlaka za tawala za Mikoa na serikali za Mitaa kupitia mabaraza hayo ya madiwani.
“Hii maana yake msingi wa kazi kubwa ya nguvu na jasho, ufundi na stadi ambao umefanywa na madiwani kote nchi nzima wakizisimamia halmashauri zetu nchini”amesema Mchengerwa.
“Hivyo niwapongeze mameya na manaibu meya, wenye viti wa halmashauri za miji na wilaya kazi yao imeandikaa katika kitabu cha dhahabu kwa sababu wamewatumikia nchi hii pamoja na wananchi wanyonge”amesema Waziri.
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Arusha ,Paul Makonda akizungumza na madiwani hao amewashukuru kwa namna ambavyo wameweza kufanya kazi kwa bidii katika kuwatumikia wananchi sambamba na kutangaza mazuri yote ya Rais Samia .
Makonda amewataka madiwani hao ambao wamemaliza muda wao wa utumishi leo rasmi kuwa chachu ya kutangaza mafanikio yote yalitofanywa katika awamu ya sita na Rais Samia Suluhu Hassan.
Makonda ameongeza kuwa , mambo yakiwa mazuri yanapeleka taswira nzuri kwa wakazi wa jiji la Arusha kuendelea kufanya kazi kwani jiji ni kitovu cha Arusha .
Aidha amewapongeza madiwani hao kwa kazi nzuri waliyoifanya kwa kuangalia kipaumbele cha Chama cha mapinduzi katika kuelekea uchaguzi mkuu.oktoba mwaka huu kama sehemu ya alama waliyoiacha kwa wananchi wao.
“Nyie mna alama ambazo hamna budi kuzifurahia kwani mmepambana sana katika kuongeza mapato kwani hiyo ni sehemu kubwa sana ya mafanikio na kupitia kikao hiki napongeza mabalozi yote ya mkoa wa Arusha kwa kazi nzuri sana ambayo mmefanya.”amesema .
Aidha amewapongeza kwa namna ambavyo wameweza kuongeza mapato ya halmashauri kwa kiwango kikubwa na kwa kufanya hivyo ni mafanikio makubwa ambayo wanapaswa kujivunia kwayo.
Makonda amesisitiza kwa Mkurugenzi wa jiji la Arusha,John Kayombo pamoja na wakurugenzi wengine katika mkoa wa Arusha kuhakikisha wanalipa stahiki za Madiwani kwa wakati ili watumie fedha hizo kwa majukumu yao ya kisiasa na mengineyo.
“Nawaomba sana mkayatangaze mema yote yaliyofanywa na serikali chini ya rais Dkt Samia Suluhu hasani ambaye amekuwa mwanamageuzi wa kiuchumi nchini.”amesema Makonda.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Joseph Mkude amewataka madiwani hao wanaomaliza muda wao kuendelea kusemea kazi za serikali zilizofanywa na Rais Samia Hassan Suluhu katika kila kata za Jiji hilo.
Amesisitiza miradi isiyokamilika serikali itasimamia ikiwemo kivuko kiaichojengwa ilhali fedha zipo kwenye akaunti kata ya Ferrari, Osunyai korongo inasemekana mkandarasi kaondoka bila kujenga hivyo yeye hatakuwa mpole, atahakikisha kazi site zilizopaswa kumalizwa zitasimamiwa
Naye Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, John Kayombo amewataka madiwani wa Jiji la Arusha kutoka kata zote 25 waliomaliza muda wao wa udiwani kutumia baraza hilo kuaga na sio kuomba miradi huku akiwashukuru kwa kazi nzuri walizozifanya ambazo watakumbukwa kwa kuweka alama .