……………..
TAASISI ya Mtetezi wa Mama imesema Rais Samia Suluhu Hassan ni kiongozi mwenye dhamira ya kweli ya kuiletea maendeleo Tanzania huku ikiwataka wananchi kuhakikisha inampigia kura za kishindo katika uchaguzi Mkuu ujao
Akizungumza mara baada ya Rais Samia kuzindua Daraja la ‘J.P Magufuli ‘ (Kigongo-Busisi) Mkurugenzi wa Taasisi ya Mtetezi wa Mama Neema Karume amesema tangu ashike usukani wa kuliongoza Taifa , Rais Samia Suluhu Hassan amefanya mambo makubwa na yenye kuacha alama.
Amesema ukiacha ujenzi wa Barabara,, Madaraja, upatikanaji wa huduma za maji , elimu, afya inayoenda sambamba na ujenzi wa Hospitali pamoja na vituo vya afya, Rais Samia amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha Tanzania inapaa kiuchumi huku akihimarisha diplomasia na mataifa mengine.
“Kuzinduliwa kwa Daraja la Kigongo- Busisi ambalo limegharimu kiasi cha zaidi ya Sh Bilioni 700, ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Msalato Dodoma na miundombinu mingine iliyokamilika na inayoendelea na ujenzi inaonesha dhamira ya kweli Kiongozi wetu kwa sisi wananchi wake” amesema Neema
Pamoja na hayo amesema Rais Samia ni kiongozi mwenye upendo kwa wananchi wake akisimamia kikamilifu ajenda ya kumtua mama ndoo kichwani pamoja na usambazaji nishati safi ya kupikia jambo lililosaidia utunzaji wa mazingira.
Aidha Mkurugenzi huyo wa Taasisi ya Mtetezi wa Mama amesisitiza kuwa wao kama watanzania wenye mapenzi mema na kupenda maendeleo, hawana chaguo jingine dhidi ya Rais Samia Suluhu Hassan katika uchaguzi Mkuu ujao kwa kuwa anatosha.
“Naomba niwasihi watanzania wenzangu kuhakikisha tunajitokeza kwa wingi katika uchaguzi Mkuu Oktoba na kumpigia kura nyingi ili aweze kupata ushindi wa kishindo, hakika anastahili kupewa heshima hiyo kwa mambo mengi na mazuri aliyoyafanya” amesisitiza Neema
Amesema Taasisi ya Mtetezi wa Mama ipo bega kwa bega na wananchi wote wapenda maendeleo na wanaounga mkono juhudi za kuliletea maendeleo Taifa zinazofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan huku akiwataka kuwaepuka na wote wanaozibeza juhudi hizo kwa kuwa ni wapinga maendeleo.
Aidha Mkurugenzi huyo amesema Octoba watetezi wa mama wote wanatick kwa Daktari Samia Suluhu Hassan kwa amani ya uhakika na maendeleo endelevu
Mwisho.