………..
Akiba Commercial Bank Plc (ACB) imewakutanisha Wateja wake Zaidi ya 150 kutoka sekta mbalimbali kuwapatia Elimu ya kifedha ili kuwasaidia kufanya maamuzi sahihi ya kifedha na kuwasaidia kukua kiuchumi.
Afisa Biashara Mkuu wa Akiba Commercial Bank Plc Bi. Wezi Mwazani akizungumza Juni 18 Jijini Mbeya wakati akifungua mkutano wa wateja ulioandaliwa na benki hiyo amesema
lengo ni kuimarisha mahusiano na kuwapa taarifu wateja kuhusu maendeleo ya Benki pamoja na fursa mbali mbali zilizopo za kuwainua wateja kiuchumi.
, Bi. Wezi Mwazani, Afisa Mkuu wa Biashara wa Benki ya Akiba, alitoa pongezi kwa mwitikio mkubwa na kusema: “Mwonekano wa ushiriki huu mkubwa unatupa faraja kuwa wateja wetu wanatuamini na wamechagua Akiba kama Benki yao pendwa. Hatuchukulii jambo hili kuwa la kawaida, na tunaendelea kujitolea kuwahudumia kwa ubora siku zote.
Bw. Humphrey Nyandindi, Meneja wa Tawi la Mbeya, alishukuru wateja kwa ushirikiano wao na kuahidi kuendelea kuwahudumia kwa bidii na kujituma Na kusema “Tunathamini sana uaminifu wenu, na tunaahidi kuendelea kuwahudumia kwa ari na moyo wa dhati ili kutimiza matarajio yenu na hata kuvuka kiwango hicho,” alisema.
Hata hivyo Mkutano kama huu ni sehemu ya mkakati mpana wa Benki ya Akiba wa kuimarisha mahusiano na wateja wake kupitia majukwaa ya majadiliano na mirejesho kutoka kwao Benki inaendelea kujikita katika kutoa huduma shirikishi za kifedha pamoja na elimu ya fedha
Naye Bw. Ntupa, Kiongozi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Soko la Mbeya, alipongeza juhudi za Benki kwa kuandaa Mkutano wenye maana kubwa, hasa kwa kuweka kipaumbele kwenye elimu ya kifedha.
“Majukwaa kama haya ni muhimu kwa maendeleo ya biashara, yanatoa maarifa kwa wateja wenu na kuimarisha uhusiano wa kuaminiana kati ya benki na jamii ya wafanyabiashara,” alisema Bw. Mtupa. Akifunga Mkutano huo