Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Tabia Maulid Mwita akibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana Zanzibar Shaib Ibrahim Muhamed huko Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe.Tabia Maulid Mwita akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud huko Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe.Tabia Maulid Mwita akitoa salamu kwa Viongozi na Watendaji mbali mbali huko Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi Dkt. Batilda Burian akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud huko Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2025, Ismail Ali Ussi akivaliswa skafu katika makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru, huko Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Wilaya ya Magharibi ‘B’.
Wakimbiaji wa Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2025 wakiwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume
……
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Tabia Maulid Mwita amewapongeza wakuu wa Mikoa na Wilaya kwa kazi kubwa wanayoifanya wakati wa mapokezi ya Mwenge wa Uhuru Kitaifa.
Mhe. Tabia ameyasema hayo wakati alipokuwa akitoa salamu kwa Viongozi mbalimbali katika makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2025 kutoka Mkoa wa Tnaga na kuenda Mkoa wa kusini Unguja huko Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume.
Aidha ametoa hamasa kwa Wananchi kushiriki katika uchaguzi Mkuu, unaotarajaiwa kufanyika Oct. Mwaka huu kwa Amani na utulivu Nchini.
Pamoja na hayo amewapongeza Viongozi wakuu wa kitaifa kwa juhudi kubwa wanazozichukuwa za kusimamia miradi mbalimbali ya maendeleo kwa Wananchi.
Akipokea Mwenge huo, Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Mohammed Mahmuod amesema jumla ya miradi minane, inatarajiwa kutembelewa na kuwekwa mawe ya msingi, yenye Thamani ya zaidi ya Sh. bilioni mia mbili katika Mkoa huo.
Huku Mkuu wa Mkoa wa Tanga Batilda Bariadi akiwapongeza Viongozi wa Jiji la Tanga kutokana na kazi nzuri walioifanya na kusema matembezi hayo yameenda vizuri katika Halmashauri zote 11 za Mkoa huo.
Kwa upande wake Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa, 2025 Ismail Ali Ussi, amesema Wananchi wameonyesha Upendo, heshima na kugusa shughuli za kijamii, ikiwemo Vijana na Mazingira.
Mwenge wa Uhuru kitaifa 2025, umezinduliwa rasmi, April 02,2025 katika Mkoa wa Pwani na Makamo wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango na unatarajiwa kufikia kilele chake Mkoani Mbea, mwezi wa 10 ,2025.
Ambapo Kauli Mbiu ya Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2025 ni “Jitokeze kushiriki Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 kwa Amani na Utulivu”.