Mlezi wa CCM mkoa wa Arusha na Katibu wa Nec Taifa itikadi na uenezi Humphrey Polepole akihutubia kufungua Darasa la itikadi kwa vijana wa vyuo na vyuo vikuu lililofanyika kwenye ukumbi wa hotel ya Naura Springs jijini Arusha
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Arusha ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro akiongea kwenya hafla ya Darasa la itikadi kwenye ukumbi wa hotel ya Naura Springs Jijini Hapa
Sehemu ya washiriki wa Darasa. La itikadi wakifuatilia kwa makini somo la itikadi lililotolewa na Katibu wa Nec Taifa itikadi na uenezi Humphrey Polepole.
Picha na Ahmed Mahmoud Arusha
……………………………………………………………………………………………………….
Na Ahmed Mahmoud Arusha.
Vijana nchini wametakiwa kusoma kwa bidii na kwa kufanya tafiti mbali mbali kwa ajili ya kulisaidia taifa kufikia adhma ya uchumi wa kati wa viwanda.
Kwa muktadha huo inabidi kujitoa kwa ajili ya kulitumikia taifa lao kwa weledi na Uzalendo ikiwa ni pamoja na kubuni vitu mbali mbali vitakavyolisadia taifa na kuacha Alama.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu wa Nec itikadi na uenezi CCM taifa Humphrey Polepole wakati akitoa mada kwenye Darasa la itikadi kwa wanafunzi wa vyuo na vyuo vikuu mkoani Arusha na kuwataka kujitokeza kuomba nafasi za uongozi.
Aliwaeleza kuwa umuhimu wa kiongozi yeyote na msomi anatakiwa kuwa mzalendo mwenye kujituma kwa maslahi ya taifa lake bila kuwa mbinafsi na anayetazama mchango wake kwa jamii.
“Viongozi waadilifu wanaanzia kwenye ngazi hii mliopo ambayo kila mmoja wenu anatakiwa kuona umuhimu wa jinsi gani ameweza kujiletea mageuzi ya kiuchumi nchi yake kwa kutumia ubunifu alionao”alisema Polepole.
Aliwataka kushiriki vizuri kutatua kero za wananchi bado wakiwa vyuoni kwa kufanya tafiti bila kusubiri uongozi ambao ni mpaka nafasi ziwepo hivyo wao wasisubiri mpaka kuambia wajitoe kwa ajili ya maendeleo ya taifa lao.
Kwa upande wake Mnec wa mkoa Arusha Daniel Awack aliwataka vijana hao kuwa sehemu ya kukusaidia taifa letu kwa kujinga maadili na nidhamu itakawasaidia kuwa sehemu ya viongozi watakao tukuka kwenye utumishi wao.
Alisema kuwa msingi wa kiongozi ni uwajibikaji na kujituma kwa lengo la kumtumikia wananchi sio kuweka ubinafsi mbele tangulizeni Uzalendo kwa taifa lenu.
Awali Katibu wa CCM mkoa wa Arusha Mussa Matoroka alisema kuwa jumuiya hiyo imekuwa chachu ya mafanikio na wanajivunia kuwa na vijana wasomi ambao watasaidia taifa na chama kuendelea kushika dola kwa kuwa na viongozi wa wasomi.