SERIKALI ya awamu ya Tano Chini ya Dakta John Pombe Magufuli imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuboresha miundombinu ya Kijamii katika Kijiji Cha Fulwe Kata ya Mikese Mkoani Morogoro ili kuhakikisha inawaondolea adha wananchi wa eneo hilo.
Kauli hiyo imetolewa na Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki ambae pia ni naibu waziri wa Kilimo Omary Mgumba wakati akiwa katika ziara ya Kijimbo katika Kijiji hicho.
Mgumba ametaja mafanikio yaliyofikiwa katika Kipindi hicho ni Pamoja ujenzi Mkubwa wa Mradi wa maji katika Kijiji cha Fulwe ambao umegharibu Zaidi ya shilingi billion mbili , jambo ambalo hivi sasa limewaondolea adha ya kutembea umbali mrefu kutafuta huduma hiyo.
Katika Sekta ya Afya Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki ambae pia ni naibu waziri wa Kilimo Omary Mgumba amesema serikali kupitia Wakala wa Barabara nchini TANROAD wanaendelea na uboreshaji wa zahanati ya Kijiji hicho.
Aidha katika Kipindi Hicho Serikali pamoja na wadau wengine wa maendeleo wameendelea kuunga mkono sekta ya elimu katika kutoa madawati pamoja na vifaa vya ujenzi ikiwemo mabati ya kuwekezea.
Katika hatua Nyingine amesema kuwa uwepo wa Kiwanda cha kuchakata mazao ya jamii ya Mikunde katika eneo la Mkambarani ambapo ni jirani na Kijiji cha Fulwe kutaibua fursa nyingi za ajira huku pia kuwepo kwa soko la uwakika la mazao hayo pamoja viungo mbalimbali
Kwa upande wao wananchi wa Kijiji cha Fulwe wameiomba serikali kumaliza adha ya ukosefu wa vyumba vya madarasa pamoja na madawati kwani inawafanya kiwango cha taaluma kushuka katika Kijiji hicho.
Akijibu hoja hiyo Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki ambae pia ni naibu waziri wa Kilimo Omary Mgumba amewataka wananchi hao kuungana na seriklai katika kauondoa changamoto hiyo na kuchana na dhana kuwa serikali imesema elimu ni bure hivyo kila kitu kitafanywa na serikali.
Mgumba amesema kuwa serikali inatoa elimu bila malipo hivyo kila mzazi bado anawajibu kushirikiana ili kuhakisha kunakuwa na mazingira mazuri ya kujifunzia kwa Watoto wao