Home Mchanganyiko TAWLA TANGA KATIKA KUELEKEA KUTIMIZA MIAKA 30 YAJIKITA KUTOA MSAADA WA KISHERIA...

TAWLA TANGA KATIKA KUELEKEA KUTIMIZA MIAKA 30 YAJIKITA KUTOA MSAADA WA KISHERIA KWA WANANCHI

0

 Mratibu wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania Mkoa waTanga(Tawla) Wakili Latifa Mwabondo akitoa elimu kwa wananchi katika Jiji la Tanga kuhusu masuala mbalimbali ya kisheria

  Mratibu
wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania Mkoa waTanga(Tawla)  Wakili Latifa Mwabondo akitoa elimu kwa
wananchi katika Jiji la Tanga kuhusu masuala mbalimbali ya kisheria

 Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi na Nyumba wilaya ya Tanga Doris Mangure kushoto akimskiliza mkazi wa Jiji la Tanga wakati wa utoaji wa huduma za msaada wa kisheria eneo la Kongwa Jijini Tanga 

CHAMA
cha Wanasheria Wanawake Mkoani Tanga (Tawla) kimeeleza kwamba wanatumia sherehe
zao za kuelekea kutimiza miaka 30 ya chama hicho kwa kutoa msaada wa kisheria,elimu na shughuli za kijamii  kwa wananchi
mbalimbali mkoani hapa kwa kuwafuata kwenye maeneo yao.
Ambapo
mpaka sasa wamekwisha kutoa elimu ya masuala ya kisheria kwa watu zaidi ya 200
ikiwemo utoaji wa msaada wa kisheria kwa watu 60.
Hayo
yalibainishwa na Mratibu wa Chama hicho mkoani Tanga Wakili Latifa Mwabondo wakati
akizungumza na waandishi wa habari ambapo alisema kwamba wamejipanga kutoa
msaada huo wa kisheria kwa jamii nzima.
“Kwa
kweli sisi kama Tawla tunaendelea kushirikiana na jamii ya wakazi wa mkoa wa
Tanga kuweza kutoa elimu kwa wananchi kwa lengo la kuwasaidia kuondosha
changamoto ambazo zimekuwa zikiwakabili hasa za kisheria”Alisema  
Alisema
kwamba tokea waanza kutoa elimu hiyo kuanzia February 1 mwaka huu mpaka
February 7  wamefanikiwa kufika katika maeneo mbalimbali ikiwemo kwenye viwanja vya Tangamano,
vyombo vya habari na shule za Changa na Usagara.
“Lakini
pia tumetoa elimu kwenye maeneo ya Kwanjeka kwa kuwafikia wakina mama pamoja na msaada wa kisheria
kwenye maeneo ya Kata ya Pongwe, Mzizima na Nguvumali na tunaamini
itawabadilisha”Alisema 
Kwa mkoa wa Tanga Tawla imekuwa ikitoa msaada wa kisheria ,elimu katika maswala mbalimbali ya kisheria  na elimu kwa njia ya mdahalo na vyombo vya habari ili kuiwezesha jamii kuweza kufahamu sheria ,haki na wajibu wao.