Home Mchanganyiko CCM KUFYEKA WAGOMBEA WANAOJIPITISHA MAJIMBONI KABLA YA WAKATI

CCM KUFYEKA WAGOMBEA WANAOJIPITISHA MAJIMBONI KABLA YA WAKATI

0

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM, Bara Philipo Mangula, akizungumza wakati alipokuwa mgeni rasmi katika Kongamano la Maadhimisho ya miaka 43, ya kuzaliwa kwa chama Cha Mapinduzi, kwa Mkoa wa Dodoma.

Mjumbe wa kamati kuu ya CCM ambaye ni Mlezi wa Mkoa wa Dodoma Bi.Leyla Ngozi,akizungumza wakati alipokuwa mgeni rasmi katika Kongamano la Maadhimisho ya miaka 43, ya kuzaliwa kwa chama Cha Mapinduzi, kwa Mkoa wa Dodoma.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi, UWT, Bi, Gaudesia Kabaka,akizungumza wakati alipokuwa mgeni rasmi katika Kongamano la Maadhimisho ya miaka 43, ya kuzaliwa kwa chama Cha Mapinduzi, kwa Mkoa wa Dodoma.

Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa Ndg.Philipo Mangula (kushoto) ambaye ni mgeni rasmi katika maadhimisho ya miaka 43 ya CCM mkoa wa Dodoma akifatilia shamrashara hizo kabla kutoa hotuba kwa wanancha wa mkoa wa Dodoma.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge, (kushoto) ambaye amehudhuria maadhimisho ya miaka 43 ya CCM  ambapo kila mkoa umeadhimisha CCM Dodoma chama na jumuiya zake zote tatu kuanzia shina,Tawi,Kata,Wilaya na Mkoa wa Dodoma akiafatilia shamrashamra.

Sheikh wa Mkoa wa Dodoma akitoa Dua kwenye maadhimisho ya miaka 43 ya CCM ambapo kila mkoa umefanya maadhimisho yake.

Mchungaji akitoa neno la Bwana kwenye Maadhimisho ya miaka 43 ya CCM ambapo kila Mkoa umefanya maadhimisho yake.

Sehemu ya viongozi na wabunge wakifatilia maadhimisho ya miaka 43 ya CCM ambapo kila mkoa umefanya maadhimisho yake.

Sehemu ya wanachama wa CCM waliofurika katika maadhimisho ya miaka 43 ya CCM Mkoa wa Dodoma wakifatilia sherehe hizo ambapo kila mkoa umefanya maadhimisho yake.

…………………………………………………………………………………………………………….

Na.Alex Sonna,Dodoma

Chama Cha Mapinduzi CCM, Kimesema hakitawavumilia wale wote wenye nia ya kugombea, katika ngazi za Ubunge na Udiwani kuanza na kujipitisha na kutoa misaada kwenye Majimbo na kata ambayo yapo chini ya viongozi wa CCM kuacha Mara moja kwa kuwa ni kosa la kimaadili ndani ya chama hicho.

Pia, wale wote ambao wanawarubuni watu kwa rushwa ili wachaguliwe, au kuanza kutumia watu kwenda kutoa misaada huku nia ikiwa ni kujisafishia njia ya kwenda kugombea kwenye majimbo au Kata hizo waache mara moja.

Hayo yamebainishwa Jijini Dodoma na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM, bara Philipo Mangula, wakati alipokuwa mgeni rasmi katika Kongamano la Maadhimisho ya miaka 43, ya kuzaliwa kwa chama Cha Mapinduzi, kwa Mkoa wa Dodoma.

Amesema ni malufuku kwa mtu yeyote mwenye nia ya kugombea kupita kwenye Majimbo au Kata ambazo zinaongozwa na CCM kuacha mara, na watakaobainika hawatasita kuyaondoa majina yao kwenye kugombea kwenye nafasi hizo, kwani mpaka Bunge litakapovunjwa rasmi ndio Majimbo hayo yatakuwa wazi.

“Rais bado ni Rais wetu, Wabunge na Madiwani bado wanatambulika katika maeneo hayo, ole wao wale wanaokwenda kujipitishapitisha huko na kutoa misaada hilo no kosa kimaadili”

“Kama katika Jimbo hilo Kuna Mbunge au Diwani wa CCM, muacheni amalize ahadi zake asibugudhiwe na mtu, Kama ni Mbunge pale litakapovunjwa Bunge pale Sasa ndio kila mtu anahaki ya kuanza michakato katika Majimbo hayo” amesema Mangula.

Aidha amewaonya wale wote ambao wamezoea kutumia rushwa kupita katika chaguzi zilizopita uchaguzi wa mwaka huu wasithubutu kwani wamejipanga kupata kuwabaini wale wote ambao wamezoea kufanya vitendo hivyo na watakaobainika hawatasita kuwaondoa katika michakato.

Pia amezungumzia uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kubainisha kuwa walijipanga katika uchaguzi huo ndio maana walishinda kwa kishindo, na kwa miaka yote wamekuwa walishinda ushindi mkubwa.

“Nawashangaa wale wanaobeza ushindi tulioupata tumeshinda kihalali na bila kuiba kura, na nashangaa wale wanaowakataa wenyeviti hao wa Mitaa waliotanana na CCM, kutokana na mipango mizuri ndio maana tulishinda” amesema.

Amesema CCM ni chama imara na uamuzi wa kuanzishwa kwa chama hicho ulifuata taratibu zote na ndio maana kipo imara na kitaendelea kuwa imara zaidi na kusimamia serikali.

Aidha ameupongeza uongozi wa Chama Mkoa wa Dodoma kwa kuendelea kutekeleza ilani ya Chama na hasa katika kusimamia miradi inayotekelezwa na Serikali kwa sababu huo ndio uhai wa Chama.

“Nimesikia kwenye ripoti yenu mmetembelea miradi 30 katika Wilaya zote za Mkoa wa Dodoma, kwa hilo niwapongeze mmefanya Jambo jema kwa uhai wa Chama chetu” amesema.

Kwa upande wake, Katibu wa CCM mkoa wa Dodoma Jamila Yusuph, akitoa maelezo kuhusu maadhimisho hayo alisema Kamati ya siasa ilifanya shughuli mbalimbali ikiwemo kutembelea na kukagua miradi 30 katika halmashauri nane zilizopo katika mkoa huo.

Amesema, licha ya kukagua utekelezaji wa ilani pia tumewafariji waliopatwa na mafuriko katika wilaya za Bahi, Chemba na Kondoa, wamewatembelea wagonjwa na wenye mahitaji maalum, waumekarabati ofisi za chama, wamefanya harambee iliyolenga kupata fedha za kukamilisha jengo la chama na kitega uchumi cha kata ya kilimani, wamepanda miti na kufanya usafi pia.

Nae mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM ambaye ni mlezi wa mkoa wa Dodoma Leyla Ngozi, akizungumza kwenye kongamano hilo amewataka wanachama kuiga utumishi uliotukuka wa mzee Mangula ambaye tangu awe mtumishi wa Chama mpaka sasa hakuna makando kando yake yoyote yaliyosikika.

Mjumbe huyo alieleza kuwa,  CCM imejipanga vyema katika mkoa huo na wapinzani hawana nafasi yoyote kwak uwa hawataruhusu jimbo lolote la mkoa huo liende upinzani.

Akitoa salamu za serikali Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dk.Binilith Mahenge, amesema idadi ya watu waliohudhuria imedhihirisha utendaji mzuri wa chama hicho katika ahadi zake ilizoziweka kwenye Ilani ya Uchaguzi ikiwemo kuhamishia serikali Dodoma.

“Pongezi kwa CCM,miaka 43 sio kidogo ni mingi sana,ndani ya nchi tunashuhudia amani,umoja na mshikamano uliosimamiwa na chama hiki,mahala pengine duniani wameshindwa kudumisha haya lakini hapa kwetu Tanzania imewezekana chini ya CCM,hongereni sana,”amesema Dkt Mahenge.

Awali Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi, UWT, Bi, Gaudesia Kabaka, amesema Serikali imefanya mambo mengi na hasa katika awamu ya tano, na kubwa zaidi hili la kufanikiwa kuhamia Dodoma, na kutokana na uimara wa Chama hicho na watapata ushindi wa Kishindo katika uchaguzi wa mwaka huu.