NASSOR KHAMIS MAELEZO 26 / 05 / 2025
Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Zanzibar ZBC Ramdhani Bukini amesema kuanzishwa kwa tamasha la usiku wa pambe kutasaidia kuutangaza utamaduni wa Mzanzibar kwani limezingatia mila, desturi na utamaduni wa Mzanzibar ambao bado unaendelea kulindwa.
Akizungumza na Waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) Rahaleo Mkoa wa Mjini Magharib amesema tamasha hilo litawashirikisha wasanii wa Taarab Asilia.
Amesema kuwepo kwa Tamasha hilo halitondoa misingi ya kihabari kwani bado wanazingatia misingi hiyo katika kuhabarisha, kuelimisha na kuburudisha jamii.
Amefahamisha kuwa tukio hilo litawahusisha wasanii wakongwe pamoja na vikundi vya Taaran Asilia kutoka Zanzibar lengo ni kuendeleza taarab hizo ili vijana waweze kujifunza kupitia tamasha hilo.
Aidha Mkurugenzi Bukini amesema ZBC imekua ikijitoa kwa jamii lengo kuiweka taasisi hiyo karibu na wanajamii ili kuendelea kuwahabarisha na kuwaburudisha.
Katika hatua nyengine amewataka wakaazi wa Zanzibar na wapenda burudani ya taarab Asilia kujitokeza katika tamasha hilo
Nao Baadhi ya Wasanii ambao watashiriki katika tamasha hilo wamefurahishwa Kwa kuanzishwa Tamasha hilo lenye lengo la kuirusha Taarab Asilia kwa jamii.
Hata hivyo wameiomba Zbc kuendeleza kwa tamasha hilo ambalo litaifanya Taarab Asilia kuwa midomoni mwa watu na kuburudisha jamii ya Zanzibar
Tamasha la Usiku wa pambe ambalo linatarajiwa kufanyika Mei 30 mwaka huu katika Ukumbi wa Hotel ya Madinat Bahar.