Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara Agness Marwa amewataka madiwani wanawake mkoani Mara kusemea kazi zilizofanywa na wabunge wa viti maalum nakuwataka kuweka pembeni toafuti za wabunge na wao wakati huu wakuelekea katika uchaguzi ambapo amewaomba kuwa sehemu ya kuzisemea kazi zilizofanywa na wabunge wao.
Agness alisema nivyema kuacha kueneza chuki baina yao badala yake wawe seheme ya kuzisemea kazi zilizofanywa na wabunge wanaomaliza muda wao nakuacha kutengeneza chuki baina yao na wabunge hao.
“Nivizuri mkasema kazi walizofanya wabunge wenu tofauti zenu tofauti zetu wekeni pembeni tunaenda kwenye uchaguzi mnatakiwa mpate Baraka msitengeneze chuki katika uchaguyzi shughulikia kitu kimoja ukiweka vitu viwili hautoweza kama kuna mtu unamuombea kura muombee ili ashinde weka chuki pembeni”Alisema Agness Marwa Mbunge wa Viti Maalum.
Pia agness amewataka madiwani hao kujitegenezea mazingira bora ya heshima wakati wanamaliza muda wao kama watahitaji kurejea nakuachana na kuingia katika mkumbo ambao utawatia doa daima kwenye maisha ya kisiasa.
Akizungumza katika Baraza la uwt katibu wa ccm mkoa wa Mara Iddy mkoa aliwatak viongozi hao kuwa wamoja kwani hawatasita kuchukua hatua kwa wale ambao wataenda kinyume na utaratibu wa chama.