Rais wa Mabunge Duniani Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa Mbeya Mjini na Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa Dkt Tulia Ackson ametangaza rasmi kugombea Jimbo la Uyole.
Ameyasema hayo katika mkutano Mkuu Maalumu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) uliofanyika katika ukumbi wa Dkt Tulia Ackson Sabasaba Jijini Mbeya.
Awali amezishukuru Kata zote thelathini na sita kwa ushirikiano mkubwa waliompatia wakati akitekeleza majukumu yake.
Unapoleta maendeleo katika jamii kuna watu wananufaika na wengine wanapata maumivu.
Aidha amesema kugawanywa kwa Jimbo ni kusogeza maendeleo kwa wananchi na maombi yalikuwa mengi nchini lakini mkoa wa Mbeya ni miongoni mwa majimbo nane yaliyogawanywa.
Wananchi wanasogezewa huduma wananchi wanasogezewa maendeleo ” amesema Dkt Tulia.
Amewahakikishia kuwa upande wowote atakaoelekea hatauacha upande mwingine kwa kuwa yeye ni mzazi wa watoto wawili.
Kwa mgawanyiko wa Jimbo la Mbeya asiwepo mtoto yeyote atakayejiona zaidi hivyo ametoa wito kwa wananchi wa Mbeya Mjini kuchagua Viongozi bora wenye hofu ya Mungu watakaochagiza maendeleo.