Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mjumbe maalum, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo (Mb.) amewasili jijini Kampala Uganda na kupokelewa na Balozi wa Tanzania nchini Uganda Mhe. Meh. Gen. Poul Kisesa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Intebbe tarehe 12 Mei, 2025.
Waziri Kombo anatarajiwa kuwasilisha Ujumbe maalumu kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluh Hassan kwa Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Gen. Yoweri Kaguta Museven.