***************************
Jeshi la polisi mkoa wa Kilimanjaro limemwachia Mchungaji Boniface Mwamposa pamoja na wenzake saba(7) kwa dhamana baada ya kuridhishwa na maelezo yao.
Akizungumza leo katika Mkoa huo SACP-Misime amesema kuwa kama ilivyokwisha kuelezwa na viongozi mbalimbali na kwenye taarifa yake ya tarehe 03.02.2020 hatua mbalimbali zinazoendelea kuchukuliwa ni kwamba baada ya tukio hilo Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania Simon Nyakoro Sirro (IGP) alituma timu ya maofisa wakiwepo wataalamu wa Uchunguzi wa Sayansi ya Jinai kwenda kuungana na timu ya wataalamu kule Kilimanjaro
katika uchunguzi.
“Katika uchunguzi huo walikamatwa watu nane (8) akiwepo Bonifase Mwamposa na kuhojiwa kwa kina na baada ya kujiridhisha na yale yaliyokuwa yanahitajika kutoka kwao wamepewa dhamana kwa mujibu wa sheria ili waendelee kuripoti wakati uchunguzi ukiendelea.
Uchunguzi bado unaendelea na baada ya kukamailika
yatakayobainika yatatolewa kwa mamlaka husika na kutelekezwa kwa mujibu wa sheria kanuni na taratibu. Hivyo kila mmoja anatakiwa awe na subira na uchunguzi unaofanywa na wataalam utakapokamilika mtajulishwa”. Amesema SACP-Misime.