Mwenyekiti wa Bodi ya TASAC Nah.Mussa Mandia akimkabidhi zawadi ya TASAC Katibu Tawala wa Wilaya ya Karagwe Rasul Shandala K wakati wa Bodi hiyo ilipotembelea Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Karagwe katika ziara ya Bodi mkoani Kagera.
Mwenyekiti wa Bodi ya TASAC Nah.Mussa Mandia akizungumza na na Wananchi wa Chamchuzi hawapo pichani wakati bodi ilipotembelea wa mwalo uliopo katika Kijiji hicho.
Mwenyekiti wa Bodi ya TASAC Nah.Mussa Mandia akizungumza na katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Karagwe wakati Bodi hiyo ilipofanya ziara ya kukagua shughuli za Mialo na Ziwa katika Wilaya hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Julius Laizer akizungumza na bodi ya TASAC iliyotembelea Ofisi yake hawapo pichani ikiwa ni ziara ya Bodi katika Wilaya hiyo.
Afisa Mtendaji wa Chamchuzi Jonas Philimaerik akizungumza na wananachi wakati wa bodi ya TASAC ilipofanya ziara katika mwalo huo.
…………
Wanannchi wa Mialo ya Chaamchuzi,Lukombe pamoja Ziwa la Lwakajunju Wilayani Karagwe wameiomba Serikali kujenga miundombinu katika mialo na Ziwa hilo ili kuweza kufanya kazi yao katika mazingira yatakayoongeza mapato ya Serikali.
Wananchi hao wameyasema hayo wakati ziara ya Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) wakati Bodi hiyo ilipotembelea mialo hiyo pamoja na Ziwa wilayani Karagwe mkoani Kagera.
Mwananchi wa Mwalo wa Chamchuzi Leonard Lupenda amesema ujio wa TASAC ni muokozi kwa changamoto zinazowakabili katika mwalo kuhusiana na kukosekana kwa gati la kuegeshea vyombo vya usafiri majini,sehemu ya abiria kupumuzikia abiria pamoja na miundombinu ya kuhifadhi mizigo katika safari zao katika nchi ya Rwanda.
Amesema kuwa mizigo wanatoa nchini Rwanda kuja Karagwe ambapo wakiweka mazingira mazuri Serikali itaongeza mapato pamoja na shughuli za uvuvi utasaidia katika kupata masoko ya samaki kutokana na miundumbinu itakayowekwa.
Kwa upende wa Jonas Bakonga amesema miundombinu katika mwalo wa Lukombe ni changamoto ikiwemo barabara ,magati ambapo serikali kuna siku itakosa mapato kwani maeneo hayo yatashindwa kufikika.
Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Kavunjo Deus Kaijage amesema kuwq suala la usalama ni changamoto na kuitaka serikali kuangalia kutokana na biashara za maeneo hayo ni kwenda katika nchi jirani hivyo wanaweza kuingia wahamiaji haramu.
Akizungumzia changamoto hizo Mwenyekiti wa Bodi ya TASAC Nah.Mussa Mandia amesema serikali inafanya kazi kubwa na kuahidi changamoto hizo zitashughulikiwa kutokana na umuhimu wa maeneo hayo katika serikali kuendelea kuongeza mapato.
Amesema kuwa ziara hiyo katika mialo hiyo pamoja na ziwa ni kuangalia usalama wa vyombo vya usafiri majini pamoja na miundombinu yake ikiwa ni kuchukua maoni ya wadau waliopo katika mnyororo huo kwa kupeleka katika ngazi mbalimbali kwa ajili ya utekelezaji.
Hata hivyo amesema kuwa katika mkoa wa Kagera kuna maziwa 15 ambapo kazi ni kuangalia juu ya shughuli zinazofanyika.
Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Julius Laizer amesema kuwa wamekuwa wakidhibiti shughuli za mageto na hawatakuwa na huruma ya majadiliano kwa mtu atakayejihusisha na mageto.
Hata hivyo amesema ujio wa TASAC ni kwenda katika kuboresha maeneo hayo ambapo ni faida kwa serikali katika kuongeza mapato yake.
Mwenyekiti wa Wasafirishaji kutoka Karagwe kwenda nchini Rwanda amesema kuwa wanaiomba Serikali kuendelea kuboresha miundombinu katika kuchochea ukusaji wa mapato na wako tayari kuendelea kushirikiana na Serikali.