Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe ametangaza kuzuia mazao ya aina yoyote kuingizwa nchini Tanzania kutoka katika nchi za Afrika Kusini na Malawi kutokana na changamoto zilizojitokeza ili kulinda biashara na wafanyabiashara wa Tanzania mpaka hapo itakavyokuwa vinginevyo, pia amezuia mazao na mbolea au mizigo yoyote ya mazao inayotoka nje ya Tanzania na kupitishwa kuelekea Malawi, amesema mazungumzo bado yanaendelea ambayo yanaongozwa na Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo.