Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) akisaini kitabu cha maombolezo katika msiba wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania miaka mingi Marehemu Hashim Lundenga ambaye alifariki Aprili 19, 2025 katika hospitali ya Kitemgule Tegeta jijini Dar es Salaam.
Mwili wa Hashim Lundenga utaagwa leo nyumbani kwake Mnara wa Voda Bunju na kusafirishwa kwao Ifakara mkoani Morogoro kwa Mazishi ambayo yatafanyika kesho Aprili 22, 2025, Mungu aiweke Mahali Pema Peponi Amen.
Pichani ni waliokuwa wadau wakubwa wa masuala ya urembo na mitindo kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB Bw. Ephraim Mafuru, David Minja na mmoja wa waliokuwa waratibu wa Kamati ya Misa Tanzania Bw. Bosco Majaliwa wakiwa katika msiba huo.
Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB Bw. Ephraim Mafuru kushoto na Bw. David Minja wakijadiliana jambo katika msiba huo.
Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete kulia Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) akizungumza Sheikh Alhadi Mussa Salum Mwenyekiti wa Kamati Amani.
Kushoto ni Basila Mwanukuzi Mwandaaji wa Miss Tanzania kwa sasa akiwa pamoja na waombolezaji wengine katika msiba huo.
Basila Mwanukuzi Mwandaaji wa Miss Tanzania kwa sasa kulia akiwa pamoja na Bosco Majaliwa aliyekuwa mratibu wa Kamati ya Miss Tanzania na waombolezaji wengine wakiwa katika msiba huo.
Aliyekuwa Miss Tanzania Nancy Sumari katikati akiwa na mshiriki mwenzie aliyewahi kushika nafasi za juu za Miss Tanzania Sophia Byanaku nao wameshiriki kikamilifu katika msiba huo.
Waombolezaji mbalimbali wakiwa katika msiba huo uliopo eneo la Bunju Mnara wa Voda jijini Dar es Salaam