********************************
NA EMMANUEL MBATILO
Shirika la reli Tanzania (TRC) limewataka wananchi, madereva wa magari na watu wanaoishi kando kando ya reli kuzingatia usalama wa reli ikiwa ni pamoja na kujiepusha na vitendo vya uharibifu wa miundombinu.
Akizungumza wakati qa uzinduzi wa kampeni ya usalama katika reli, Kaimu mkurugenzi wa TRC, Bw. FOCUS SAHANI amesema kuwa ili kuimarisha usalama katika reli inapaswa kila mwananchi na wadau binafsi kutoa taarifa za vitendo vya hujuma hizo polisi na kuhakikisha wahujumu hao wanachukuliwa hatu za kisheria.
“Mara kadhaa kumekuwa na matukio ya baadhi wananchi wasio raia wema wanajaribu kuiba ama kufanya hujuma kwa kutega vyuma relini.Serikali inatambua katika maeneo hayo wanakojaribu kuhujumu ama kutega treni,wapo raia wema”. Amesema Bw.Sahani.
Kaimu kamishina wa jeshi la polisi kikosi cha usalama wa reli Stanley kulyamo amesema kumekuwa kikosi hicho tayari kinawashikilia watu kadhaa kutokana na makosa ya uharibifu wa miundombinu ya reli na uchunguzi utakapokamilika watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabiri.
Nae Mwanasheria wa TRC VERONICA SUDAI amesema adhabu ya kuhujumu miundombinu ya reli ni pamoja na faini isiyopungua Milioni 50, ama kifungo kisichopungua miaka 3.
Mkuu wa usalama wa reli Mahizo martini mgezi amesema Madhara ya ajali za treni ni makubwa kutokana na kubeba watu wengi kwa wakati mmoja hivyo kuwahimoza wananchi kujiepushe na wizi wa mataruma na hujuma nyinge ili kuhakikisha usalama wa reli na treni unakuwepo.