Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Ndg. Stephen Wasira akilipa fedha taslim kwa Muuzaji wa Vifaa vya Chama mara baada ya kununu kofia (aliyoivaa kichwani) akielekea katika Ukumbi wa Kanisa kuzungumza na Wanachama wa CCM na Viongozi Mbalimbali wilaya ya Mbozi, Leo Machi, 14, 2025.

Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Ndg. Stephen Wasira akilakiwa na Vikundi vya ngoma akiwasili katika Ukumbi wa Kanisa kuzungumza na Wanachama wa CCM na Viongozi Mbalimbali wilaya ya Mbozi, Leo Machi, 14, 2025.


VIONGOZI na wanachama wa CCM Mkoa wa Songwe wakicheza na kushangilia walipokuwa wakimkaribisha Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Stephen Wasira katika Ukumbi wa Kanisani, Vwawa wilayani Mbozi Mkoa Songwe.



Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Stephen Wasira akizungumza na wana CCM katika ukumbi wa Kanisani Vwawa Wilaya Mbozi mkoani Songwe akiwa kaika ziara ya kikazi kukagua uhai wa Chama na Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi

Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo akiwasilisha tarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika mkutano wa ndani ikiwa sehemu ya ziara ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Stephen Wasira katika Ukumbi wa Kanisani Vwawa, Wilaya Mbozi mkoani Songwe.