Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimeanza Warsha ya mafunzo ya uongozi kwa viongozi wa chama hicho imeanza rasmi leo katika ikiwakutanisha Wajumbe wa Kamati Kuu, Sekretarieti ya Kamati Kuu, Makatibu wa Kanda na Viongozi wengine wa chama.
Warsha hii inalenga kuwawezesha viongozi hao kuwa mbinu bora za uongozi, usimamizi wa rasilimali na maamuzi yenye tija kwa chama na jamii kwa ujumla.
Mafunzo haya yanaendeshwa na wakufunzi waliobobea katika uongozi na usimamizi wa masuala ya kitaasisi, wakiwemo Mwenyekiti wa Chadema taifa Tundu Lissu Profesa Mussa Assad Aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Philbert Kumu na Muhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Mwendeshaji wa warsha hii ni Julius Mwita, ambaye atahakikisha washiriki wanapata maarifa muhimu kwa ajili ya kuimarisha uongozi ndani ya chama.
Katika siku ya kwanza ya warsha, washiriki wamejadili mada mbalimbali zinazohusu uongozi, uwajibikaji na usimamizi wa rasilimali za chama, huku wakipata nafasi ya kuuliza maswali na kushiriki mijadala yenye tija.
Warsha hii inaendelea kwa siku kadhaa ambapo mada zaidi zitajadiliwa, ikiwa ni sehemu ya juhudi za chama kujenga uongozi thabiti na wenye tija kwa maendeleo ya wananchi.