Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Coletah Kokutangilila (kushoto) na Simon Mollel, watumimishi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) wakati alipotembelea banda la maonesho la NIDA kabla ya kufungua Kongamano la Wanawake Kanda ya Kusini kwenye Uwanja wa Maegesho, Nachingwea mkoani Lindi, Machi 6, 2025. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Amon Mpanju na wa tatu kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Zainab Telack. (Picha na Ofisi ya Waziri MNkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama mchapisho mbalimbali alipotembelea banda la maonesho la Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kabla ya kufungua Kongamano la Wanawake Kanda ya Kusini lililofanyika kwenye Uwanja wa Maegesho, Nachingwea Mkoa wa Lindi, Machi 6, 2025. Wa pili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Zainab Telack na wengine kutoka kushoto ni Watumishi wa TAKUKURU, Theodora Paschal, Emma Mwasyege na Deborah Nkwabi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Stella Andrea kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) Naliendele ambaye alitoa maelezo kuhusu miche ya zao la korosho wakati Waziri Mkuu alipotembelea banda la maonesho la TARI kabla ya kufungua Kongamano la Wananwake Kanda ya Kusini lililofanyika kwenye Uwanja wa Maegesho, Nachingwea Mkoani Lindi, Machi 6, 2025. Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Lindi, Zainab Telack. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi alipowasili kwenye uwanja wa Ndege wa Nachingwea na baadae alifungua Kongamano la Wanawake Kanda ya Kusini lililofanyika kwenye uwanja wa Maegesho, Nachingwea mkoani Lindi, Machi 6, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Wananchi wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipofungua Kongamano la Wanawake Kanda ya Kusini lililofanyika kwenye uwanja wa Maegesho, Nachingwea Mkoani Lindi, Machi 6, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)