Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) Prof. Mark Mwandosya (katikati) akipokea zawadi ya mfuko kutoka kwa Meneja Usalama Mahala pa Kazi wa Kampuni ya Kuhifadhi Mafuta Tanzania (TIPER), Bi. Leah Wandwi, baada ya kutembelea banda la kampuni hiyo wakati wa Mkutano na Maonesho ya 11 ya Petroli ya Afrika Mashariki (EAPCE’25) unaoendelea jijini Dar es Salaam. Pamoja nao ni Mhandisi Edgar Njeje wa TIPER.
Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dkt.James Andilile,akiendesha Mada kuhusu Ushawishi wa Siasa za Kikanda kwenye Mahitaji na Bei ya Mafuta, leo 6/3/2025 kwenye Mkutano wa 11 wa Mafuta na Gesi Asilia Afrika Mashariki unaoendelea katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere.