

Happy Lazaro,Arusha .
Arusha .Mamlaka ya udhibiti wa mbolea Tanzania imejiwekea
malengo ya kusajili wakulima milioni saba kwa nchi nzima kufikia mwisho wa mwezi julai 2025 ambapo hadi sasa wameshasajili wakulima million 4.4M ( 4,369.010) ambapo ni sawa na asilimia 62.4% ya malengo tuliyojiwekea kama Mamlaka kwa nchi nzima.
Aidha mamlaka hiyo pia imejiwekea malengo ya kusajili wakulima 1,790,594 kwa kanda ya kaskazini ambapo hadi sasa hivi wameshasajili wakulima 553,101 ambapo ni sawa na asilimia 31% ya malengo.
Hayo yamesemwa na Afisa udhibiti ubora kanda ya kaskazini ,Lydia Kalala wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda lao katika kuelekea maadhimisho ya siku ya wanawake duniani machi 8 mwaka huu.
Amesema kuwa, serikali ya awamu ya sita iliamua kutoa ruzuku ya mbolea kuanzia mwaka 2022/2023 ambapo utekelezaji wake unafanyika kwa mfumo wa kidijitali wa mbolea .
“mategemeo yetu tuna Imani kwa kasi tunayoenda nayo sasa baada ya kuongeza ushirikiano na kwa kushirikiana na halmashauri zote 32 za kanda ya kaskazini ,malego tutayafikia vema sana na kwa wakati.
Amefafanua kuwa ,kumekuwa na ongezeko la usajili wa wakulima kwa mwaka
2022/2023 wastani wa kasi ya usajili wa wakulima ulikuwa mdogo sana
ukifananisha na 2024/2025.Kanda ya kaskazini tulikuwa tumesajili wakulima 400,000 hadi mwezi Novemba 2024, ambapo katika 2024/2025 tumeshasajili wakulima 553,101 na zoezi la
usajili bado linaendelea.
Aidha amesema kuwa,hata Wastani wa usajili kwa wiki umepanda kutoka kusajiliwakulima chini ya 2000/wiki, hadi kufikia wastani wa kusajili wakulima 8000/wiki kwa sasa ambapo hizo ni jitihada kubwa sana zinazofanywa na Wizara ya Kilimo kupitia Mamlaka ya udhibiti wa
Mbolea Tanzania.
“Kasi hii imechagizwa na mafunzo yaliyotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania kwa kutoa elimu kwa maafisa ugani na watalaamu wa kilimo nchini kutumia Vishikwambi vilivyogaiwa na Wizara ya Kilimo Kuvitumia kwa kusajili wakulima katika ngazi ya Kijiji,Kata ili waweze waweze kunufaika na ruzuku ya mbolea na mbegu .”amesema .
Amefafanua kuwa usajili wa mkulima kwa kutumia kishikwambi umerahisisha zoezi ambapo mkulima anasajiliwa ndani ya dakika 5 na kupata namba
yake ya kuchukua mbolea ambapo hii imerahisha muda,na imempunguzia mkulima umbali wa kwenda
kujisajili na pia imeongeza usahihi wa taarifa za mkulima kwa sababu anayemsajili mkulimani
afisa ugani ambaye anasimamia kata au Kijiji husika kama aneo lake la kazi.
Aidha kwa kanda ya Jumla ya wataalamu 973 wa kanda ya kaskazini walipatiwa mafunzo kwa njia ya mtandao(Zoom meeting) na mubashara.
Amesema kuwa,Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inamjali Mkulima ambapo kwa mwaka huu wa fedha 2024/2025 imeanza utekelezaji wa Mradi wa Kadi Janja wenye lengo la kutoa kadi hizo kwa wakulima ili kurahisisha michakato ya huduma mbalimbali kwa wakulima; ikiwemo upatikanaji
wa huduma za kifedha kwa wakulima, Ruzuku ya pembejeo, na uwezeshaji wa wakulima katika kuwapatia hati miliki za mashamba yao.
“Lengo kuu la mradi huu ni kuiwezesha Serikali na taasisi zinazotoa Huduma za Kifedha kurasimisha shughuli za kilimo kuwa za kibiashara zaidi, kuongeza uwazi, na kuendeleza mbinu endelevu za kilimo
Mradi huu unatekelezwa kwa kuunganisha taarifa za wakulima katika mfumo wa kidijitali na kuziunganisha na huduma za kununua pembejeo za kilimo.
Aidha, utekelezaji wa mradi huu umeanza kwa mikoa ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini kwa kuwa na pilot katika mkoa wa Songwe na Mbeya.
Amesema kuwa ,TFRA inatambua thamani ya mwanamke na mchango wa mwanamke katika jamii na utumishi wa umma,hivyo basi ametoa wito kwa wanawake wajue biashara ya mbolea ni biashara kama biashara zingine,hivyo wanawake wanakaribishwa sana kujihusisha na biashara ya mbolea ili kuongeza jitihada katika kuinua tasnia ya kilimo katika nchi yetu ya Tanzania.
“Natoa wito kwa wakulima kuendelea kujisajili kupitia kwenye mfumo wa ruzuku ambapo zoezi hili linaendelea
katika ngazi za vijiji na kata,mtafute mtaalamu wa kilimo wa kijijini kwako atakusajili na utaweza kupata namba ya kuchukulia mbolea.”amesema.