Mkurugenzi Mkuu wa TPHPA ,Profesa Joseph Ndunguru wakati akizungumza katika uzinduzi wa nyimbo hizo mkoani Arusha

Mkurugenzi Mkuu wa TPHPA ,Profesa Joseph Ndunguru wakati akizungumza katika uzinduzi wa nyimbo hizo mkoani Arusha
Happy Lazaro, Arusha.

Paroko wa parokia ya Mtakatifu Yuda Tadei Muriet, Sandra Abraham Jinu akizungumza katika uzinduzi huo mkoani Arusha .
………….
Jamii nchini imetakiwa kuwa mstari wa mbele kuchangia maswala ya maendeleo pamoja na kuwaunga mkono watu wenye mahitaji ili waweze kuondokana na changamoto mbalimbali.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa TPHPA ,Profesa Joseph Ndunguru wakati akizungumza katika uzinduzi wa nyimbo tatu za injili za kwaya ya Mtakatifu Rita wa Kashia Muriet Parokia ya Mtakatifu Yuda Tadei Muriet mkoani Arusha .
Profesa Ndunguru ambaye ni mlezi wa kwaya hiyo amesema kuwa, ni.vizuri jamii ikawa mstari wa mbele katika kuchangia na kuunga mkono maswala mbalimbali yakiwemo ya Mungu ili injili iweze kwenda mbele .
Ameongeza kuwa ,uwepo wa nyimbo hizo za injili katika sehemu mbalimbali zimekuwa zikisaidia sana kuhubiri amani katika maeneo ambayo hayajafikiwa na huduma hiyo ,hivyo endapo tutawaunga mkono itasaidia sana kuwafikia ambao hawajafikiwa na huduma hiyo.
Aidha uzinduzi wa nyimbo hizo umeenda sambamba na uzinduzi wa Mfuko wa Rita Charity ambao utatumika kusaidia watu wenye mahitaji mbalimbali .
Aidha ametaja nyimbo hizo kuwa ni pamoja na wimbo wa Tawala bwana ambao umebeba jina la Profesa Ndunguru wimbo mwingine ni Upendo wa Mungu,na wimbo wa tatu ni Hubirini ambapo bado wanaendelea kurekodi nyimbo mbalimbali .
Kwa upande wa mgenirasmi katika uzinduzi wa nyimbo hizo ,Mkurugenzi wa kampuni ya Plant Biodefender kutoka mkoani Kilimanjaro ,Dokta Neva Zekeya amesema kuwa,kitendo kilichofanywa kinapaswa kuungwa mkono na wadau mbalimbali kwani ni jambo kubwa na baraka katika jamii .
Aidha ameongeza kuwa,kila.mmoja ana nafasi yake na kamwe wasjisifu kwa nafasi hiyo kila mmoja afanye wajibu wake.
“Mna maono mazuri ya kujitolea na nimeona mnataka kuwa wanakwaya mnaojimudu kiuchumi,na nawaombeni sana mtumie nafasi yenu vizuri kufikisha ujumbe hususani katika kuhubiri amani”amesema.
Aidha katika uzinduzi huo mgenirasmi amechangia kiasi cha shs 3.5 ambazo amenunua flash kwa ajili ya kuchangia huduma hiyo isonge mbele.
Naye Mwenyekiti wa kwaya hiyo Jonas Ngowi amesema kuwa katika uzinduzi huo wanatarajia kukusanya kiasi cha shs 50 milioni kwa ajili ya uendeshaji wa kwaya hiyo na kuweza kusaidia mahitaji mbalimbali .
Ngowi amesema kuwa, mahitaji ya kwaya hiyo ni kununua kinanda,ngoma ,power mixer ,spika mbili kubwa,Amplifaya,vishikwambi 25 pamoja na kinanda kidogo .
Ngowi amewataka wadau mbalimbali kuendelea kushirikiana kwa pamoja katika kuchangia kwaya hiyo ili waweze kufikia malengo yao ya kupeleka huduma katika maeneo mbalimbali .
Akizungumza katika uzinduzi huo Paroko wa parokia ya Mtakatifu Yuda Tadei Muriet, Sandra Abraham Jinu amesema kuwa ,amewataka wananachi mbalimbali kuwa mstari wa mbele katika kusaidia maswala hayo kwani kwa kufanya hivyo wanamkopesha Mungu.