Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis amesema hayo wakati akitoa salamu za rambirambi wakati wa Ibada ya kuuaga mwili wa Marehemu Bi. Sifaeli Mushi, aliyeshiriki tukio la kuchanganya udongo wa Muungano iliyofanyika katika Kanisa la Kiinjili la
Kilutheri Tanzania (KKKT) Machame wilayani Hai Mkoa wa Kilimanjaro leo
tarehe 26 Februari, 2025. Marehemu Bi. Sifael ambaye alifariki dunia tarehe 20 Februari, 2025 jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis akiwa na viongozi mbalimbali akishiriki Ibada ya kuuaga mwili wa Marehemu Bi. Sifaeli Mushi, aliyeshiriki tukio la kuchanganya udongo wa Muungano iliyofanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Machame wilayani Hai Mkoa wa Kilimanjaro leo tarehe 26 Februari, 2025. Marehemu Bi. Sifael ambaye alifariki dunia tarehe 20 Februari, 2025 jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis akiweka shada la maua wakati wa maziko ya mwili wa
Marehemu Bi. Sifaeli Mushi, aliyeshiriki tukio la kuchanganya udongo wa Muungano, mara baada ya ibada iliyofanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Machame wilayani Hai Mkoa wa Kilimanjaro leo tarehe 26 Februari, 2025. Marehemu Bi. Sifael ambaye alifariki dunia tarehe 20 Februari, 2025 jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis akikabidhi picha yenye taswira ya tukio la kuchanganya udongo wa Muungano kwa mwanafamilia ya Marehemu Bi. Sifaeli Mushi, ambaye alishiriki tukio hilo, mara baada ya maziko nyumbani kwa marehemu Machame wilayani Hai Mkoa wa Kilimanjaro leo tarehe 26 Februari, 2025. Marehemu Bi. Sifael ambaye alifariki dunia tarehe 20 Februari, 2025 jijini Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Christina Mndeme na katikati ni Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanznaia (KKKT) Frederick Shoo.

………….

Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais imesema inatambua na kuthamini mchango wa walioshiriki katika kuasisi na kuudumisha Muungano hususan wakati tukio la kuchanganya udongo wa Tanganyika na Zanzibar. 

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis amesema hayo wakati akitoa salamu za rambirambi wakati wa Ibada ya kuuaga mwili wa Marehemu Bi. Sifaeli Mushi, aliyeshiriki tukio la kuchanganya udongo wa Muungano, katika Ibada ya mazishi iliyofanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Nkwarungo Machame wilayani Hai Mkoa wa Kilimanjaro leo tarehe 26 Februari, 2025. Marehemu Bi. Sifael alifariki dunia tarehe 20 Februari, 2025 jijini Dar es Salaam.

Mhe. Khamis, amemwelezea Bi. Sifael Mushi kuwa, alikuwa mzalendo ambaye hakusita wakati wote kueleza mazuri yote na faida za Muungano huu adhimu hususan kwa vijana ili kuulinda na kuutetea.

“Bi. Sifaeli alikuwa ni mmoja wa vijana walioshiriki tukio la kuchanganya udongo wa Tanganyika na Zanzibar lililofanyika tarehe 26 Aprili, 1965 katika sherehe za mwaka mmoja wa Muungano zilizofanyika katika Uwanja wa Uhuru, Jijini Dar es Salaam. Alishiriki katika tukio hilo akiwa kijana mwenye umri wa miaka 32 pamoja na wenzake watatu (Mzee Hassan Omari Mzee kutoka Zanzibar, Bi. Khadija Abasi Rashid kutoka Zanzibar na Bw. Hasanieli Elisaeli Mrema kutoka Tanzania Bara),“ amesema Naibu Waziri. 

Amesema kwa kutambua mchango huo, Ofisi ya Makamu wa Rais pia iliwahi kuwaalika wazee hao Bungeni wakati wa kusoma hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Rais tarehe 3 Mei, 2016 na walishiriki ambapo tukio la mwisho ambalo alishiriki na wenzake watatu ni Maadhimisho ya miaka 54 ya Muungano katika Uwanja wa Jamhuri, Dodoma tarehe 26 Aprili, 2018, tukio hili aliweza kushiriki na wenzake wote watatu.

Halikadhalika, Mhe. Khamis amesema Serikali inatambua mchango mkubwa wa wazee hao wanne ambao wote ni marehemu, hivyo mwaka 2014 walitunukiwa Nishani ya Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Muungano Daraja la Nne. Nishani hizi zilitolewa na Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano, Awamu ya Nne katika Hafla iliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam tarehe 26 Aprili, 2014.

Aidha, Naibu Waziri amewasilisha salamu za pole kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na salamu kutoka wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango.

Akitoa salamu zake Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini ya KKKT Frederick Shoo ambaye aliongoza ibada ya kumuaga Marehemu Sifael aliwataka Watanzania kuwekeza katika elimu.

Alisema ni muhimu kuiga mazuri ya marehemu hususan katika suala la elimu ambalo aliitumikia kwa moyo wote katika kipindi cha uhai wake wakati anafundisha wanafunzi.

Mara baada ya ibada hiyo mwili wa Marehemu ulipelelekwa nyumbani kwake kwa ajili ya maziko ambayo yalihudhuriwa na ndugu, jamaa na wananchi mbalimbali.