……………….
Na Sixmund Begashe
Timu ya Riadha ya Wizara ya Maliasili na Utalii (MNRT RUNNERS) leo imeshiriki katika mbio za hiyari Mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro zijulikanazo kama “KILIMANJARO INTERNATIONAL MARATHON” msimu wa 23 kwa lengo si tu la kuhamasisha watumishi wa umma kuimarisha afya zao kupitia michezo bali pia kuitangaza Wizara hiyo yenye mchango mkubwa katika uhifadhi wa Maliasili na Utalii nchini.
Aidha, wakimbiaji hao walizipamba mbio hizo kwa jezi za Wizara hiyo kupitia Mradi wa Kuboresha Usimamizi wa Maliasili na Kukuza Utalii Kusini mwa Tanzania (REGROW) hali iliyopongezwa na wengi kwa kuwa zilikuwa na maandishi ya kutangaza maeneo ya Utalii nchini.
Akizungumza kwa niaba wa wachezaji wa MNRT Runners, Kapteni wa timu hiyo Bw. Elibariki Buko, ameushukuru uongozi wa Wizara hiyo kwa kuendelea kuhamasisha watumishi wake kufanya mazoezi kwa afya zao na kuwaasa kuendelea kuitangaza Wizara kupitia Matamasha ya Michezo ya kitaifa na Kimataifa kwa maslahi mapana ya Uhifadhi na Utalii endelevu nchini.
Mbio hizo zilizo ongozwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko zilishirikisha zaidi ya washiriki 15,000 kutoka kwenye nchi 59 Duniani kwa umbali wa kilomita 42, 21 na 5, zimekuwa zikifanyika kila mwaka, Mkoani Kilimanjaro, huku MNRT Runners wameshiriki mbio za umbali wa Kilomita 21